ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 9, 2018

Mbarawa azindua vichwa vya treni na kutaka mpangokazi TAZARA

 Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa TAZARA pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao pamoja na uzinduzi wa vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Chingandu Bruno akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao pamoja na uzinduzi wa vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.


 Mshehereshaji Masoud Masoud akiwapitisha kwenye ratiba mgeni rasmi na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao pamoja na uzinduzi wa vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu wa Mkoa wa Tazara nchini, Fuad Abdallah akitoa maelezo kwa Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na wa wageni waalikwa kuhusu mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao kutoka Dar es Salaam hadi Kapiri Mposhi nchini Zambia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo ulioambatana na kuzinduza vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao kutoka Dar es Salaam hadi Kapiri Mposhi nchini Zambia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo ulioambatana na kuzinduza vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Mkuu wa Mkoa wa Tazara nchini Fuad Abdallah (kushoto).
 Meneja Mkuu wa Mkoa wa Tazara nchini, Fuad Abdallah (katikati) akimuelekeza mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa jinsi mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao kutoka Dar es Salaam hadi Kapiri Mposhi nchini Zambia unavyofanya kazi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo ulioambatana na kuzinduza vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mshehereshaji Masoud Masoud.
 Meneja Mkuu wa Mkoa wa Tazara nchini, Fuad Abdallah akielezea mfumo huo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao unavyofanya kazi kwa mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo ulioambatana na kuzinduza vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia kwa umakini ‘presentation’ ya mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao unavyofanya kazi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo ulioambatana na kuzinduza vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
 Mabehewa 10 ya kokoto pamoja na vichwa viwili vya treni vilivyozinduliwa na Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwenye hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TAZARA na wageni waalikwa walishiriki uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao pamoja na uzinduzi wa vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya viongozi wa TAZARA na viongozi wa vyama vya wafanyakazi waliohudhuria uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao pamoja na uzinduzi wa vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya mafundi walioshiri kukarabati mabehewa hayo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao pamoja na uzinduzi wa vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na kuabadilishana mawazo na baadhi ya wateja wanaotumia huduma ya TAZARA kusafirisha mizigo yao wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao pamoja na uzinduzi wa vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa TAZARA na wageni waalikwa wakishuhudia moja kati ya vichwa viwili vya treni vilivyozinduliwa rasmi na Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakati wa hafla iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiingia kwenye moja kati ya vichwa viwili vya treni vilivyozinduliwa rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao uliombatana na uzinduzi wa vichwa viwili vya treni na mabehewa hayo uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akikata utepe kwenye moja kati ya behewa kumi za kototo zilizokarabatiwa nchini wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao pamoja na uzinduzi wa vichwa viwili vya treni na mabehewa hayo uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi wetu,
WAZIRI wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia - Tazara, kutengeneza mpango kazi utakaowezesha kununua vichwa viwili vya treni katika mwaka mmoja.

Alisema wakishatengeneza mpango kazi huo wamfikishie ofisini auangalie.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa vichwa viwili vya treni na mabehewa kumi ya kokoto yaliyokarabatiwa na wataalamu wa ndani na kuokoa mabilioni ya shilingi.

Ukarabati huo uligharimu sh milioni 167 huku vichwa na mabahewa hayo vikiwa na vina uwezo wa kuendelea kutumika kwa miaka 15 hadi 20.

Imeelezwa katika  uzinduzi huo kwamba mabehewa hayo yalikuwa yameharibika na kuacha kutumika miaka 10 iliyopita wakati vichwa hivyo vilipata ajali na kuharibika kiasi cha kushindwa kurejea kazini.

Aidha Mbarawa alisema kwamba kama mabehewa hayo kumi na vichwa viwili ingebidi kununuliwa upya Mamlaka hiyo ingetumia shilingi bilioni 17.

Pamoja na kuwapongeza kwa uzalendo na kazi nzuri iliyofanywa, Waziri huyo aliisisitizia mamlaka  kutengeneza mpango kazi utakaoiwezesha kupata shilingi za kitanzania bilioni 7 ili kupata vichwa vipya vya treni.

Katika hotuba yake alisema anaamini hizo fedha zinaweza kupatikana kwa kuondoa matumizi yasiyo ya lazima katika mamlaka hayo.

“Tazara tukate matumizi yasiyokuwa na msingi, Tazara isimame vyema…” alisema na kuongeza kuwa kwa kufanya maamuzi hayo ya msingi na kwa ushirikiano na serikali mambo yataenda vyema.

Alisema imekuwa ni kawaida kwa taasisi za serikali zinazofanya biashara kusubiri serikali kwa kila kitu jambo ambalo si jema na kwa kuwa Tazara imeonesha inaweza kwa ukarabati uliofanywa kwa vichwa na mabehewa, inachotakiwa sasa ni kujipanga.

Alisema mamlaka hiyo ambayo hadi sasa ina vichwa 10 vya treni inahitaji vitendea kazi ili iweze kufikia ufanisi hasa katika usafirishaji wa mizigo ambayo ndiyo inayoleta faida kwa mamlaka.

Alisema usafirishaji wa abiria ni huduma kwa hiyo ni vyema kuwa na vitendea kazi vya kutosha ili kukidhi mahitaji ya ushindani.

Akizungumza na wafanyakazi baada ya uzinduzi wa vichwa na mabehewa hayo pamoja na mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji mizigo kwa njia ya mtandao kutoka Dar es Salaam hadi Kapiri Mposhi nchini Zambia, alisema kwamba wakati umefika wa kufumua mfumo wa utawala na kubakisha watu wachache katika kada ya juu.

Alisema ipo haja ya mfumo kubadilika kwa kuzingatia mahitaji ya sasa badala ya kubaki na mfumo wa menejimenti wa kizamani katika mahitaji mapya.

Aliwataka pia watendaji wanaoangalia mfumo wa usafirishaji wa kielektroniki unaopatikana  katika Programu iliyopo kwenye simu ya mkononi ambao umetengenezwa na mamlaka yenyewe bila kuagiza toka nje, kuhakikisha mfumo huo hauhujumiwi na wao wenyewe wanajua namna ya kuutumia.

Alisema kuna wakati alifika Posta na kugundua kwamba mfumo wa pili wa uangalizi umehujumiwa kwa kuwa viongozi wenyewe walikuwa hawaujui.

Akielezea mfumo huo Meneja Mkuu wa Mkoa wa Tazara nchini Fuad Abdallah alisema kwamba mfumo huo wa kielektroniki utawawezesha wafanyabiashara wanaotumia huduma yao kujua mizigo yao ipo wapi kupitia program inayopatikana kwa watumiaji wa simu zenye mfumo wa Androidna Ios.

Pia itawezesha mamlaka kujua mwenendo wa treni zake, njia pamoja na matumizi ya nishati kwa kuangalia chati za madereva.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Chingandu Bruno alisema mamlaka hiyo imepata mafanikio makubwa sana katika utendaji wake hasa kwa kukarabati vichwa hivyo na mabehewa na pia kupungua maeneo ya hatari katika njia kutoka 51 hadi 21.

Maeneo hayo yalikuwa yanahitaji dreva wa treni kupunguza spidi na hivyo kuchelewesha muda pangwa wa kufika wa safari.

Aidha wamepunguza muda wa kushughulikia mizigo ya wateja wao.

Meneja huyo pia aliwapongeza wafanyakazi wa mamlaka hiyo kwa kujituma na kusema kama si juhudi za wafanyakazi wazalendo mamlaka hiyo ingekuwa na shida kubwa ya kuwa na vitendea kazi.

No comments: