Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
BALOZI wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki kwa niaba ya Makao Makuu ya Jeshi amemvisha rasmi Kanali R.C Ng’umbi cheo kipya cha Brigedia Jenerali.
Brigedia Jenerali Ng’umbi ambaye pia ni Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Tanzania nchini China , ni miongoni mwa maofisa 27 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopandishwa vyeo tarehe 12 Aprili mwaka ,2018 na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Magufuli.
Akizungumza Mara baada ya kuvalishwa Cheo hicho jana Mei 7 , Brigedia Jenerali alimshukuru Amiri Jeshi Mkuu Dk. Magufuli pamoja na uongozi wa Makao Makuu ya Jeshi kwa kupandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali.
Tukio hilo lilifanyika katika ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini China na kuhudhuriwa na maofisa pamoja na watumishi kutoka ofisi za Ubalozi pamoja na familia zao.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki kwa niaba ya Makao Makuu ya Jeshi akimvisha rasmi Kanali R.C Ng’umbi cheo kipya cha Brigedia Jenerali katika hafla iliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania nchini China.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, Brigedia Jenerali, R.C Ngumbi wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China.
Brigedia Jenerali R.C Ngumbi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mbelwa Kairuki, Maafisa na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China.
No comments:
Post a Comment