ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 9, 2018

Waziri Mwakyembe afungua Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi

 Mnadhimu Mkuu; Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed akizungumza wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mnadhimu Mkuu; Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na mchezaji wa Timu ya  Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipokua akikagua timu hiyo wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Makao Makuu ya Jeshi wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu - WHUSM

Na Genofeva Matemu- WHUSM
Timu za majeshi kupitia michezo mbalimbali zimetakiwa kuweka mikakati na kuibua wanamichezo wazuri ambao wataiwakilisha vyema nchi katika mashindano ya kimataifa na kuleta ushindi na medali mbalimbali kama ilivyokuwa hapo zamani.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) katika uwanja wa uhuru jana Jijini Dar es Salaam

“Ni matarajio yangu kuwa uwepo wa michezo hii inaashiria azma na nia thabiti ya kurejesha enzi  za majeshi yetu kutoa uwakilishi ulio mzuri katika michezo ndani na nje ya nchi kama ilivyokuwa hapo zamani” amesema Mhe. Mwakyembe

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed amesema kuwa kufanyika kwa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi kila mwaka kunathibitisha azma ya JWTZ kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini kwa kuunda timu za JWTZ zitakazotumika kuimarisha timu mbalimbali za Taifa katika mashindano ya Kimataifa. 
Jenerali Yakubu amesema kuwa uwepo wa michezo ya majeshi katika jumuiya ya Afrika Mashariki umekua nyenzo ya kudumisha amani baina ya nchi wanachama hivyo wachezaji watakaopata fursa kushiriki michuano hiyo washiriki vema na kuleta tija kupitia michezo hiyo. 


Mashindano ya Muula wa tano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) yenye kauli mbiu isemayo “Tushiriki Michezo kama sehemu ya kazi, Kulinda   Afya zetu na kudumisha mshikamano” yataendana na uteuzi wa wanamichezo watakaoteuliwa kuunda timu za JWTZ zitakazoshiriki mashindano tarajiwa ya Majeshi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huko nchini Kenya mwaka 2019.

No comments: