Advertisements

Thursday, June 14, 2018

Eid al-Fitr 2018: Ni lini, Waislamu duniani wanaisherehekeaje na kwanini tarehe hubadilika?


 Na Jumia Travel Tanzania


Ni utamaduni wa kawaida kwa waumini wa dini ya Kiislamu duniani kote kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr kuashiria kuisha kwa kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa lugha ya Kiarabu neno Eid al-Fitr lina maana ya “sherehe ya ukomo wa mfungo” tukio ambalo hukusanya jamii ya Waislamu wote duniani kujumuika na kusherehekea kuisha kwa tukio hili muhimu la kiimani ndani ya mwaka.


Ingawa tukio hili huwa linafanyika kila mwaka lakini Jumia Travel imekukusanyia yafuatayo ambayo huna budi kuyafahamu kuhusu sherehe hizi.

Eid ni lini?


Tarehe rasmi ya Eid bado haijafahamika kwa kuwa inategemeana na mzunguko wa mwezi lakini tunajua kwamba kuna uwezekano mkubwa ikawa kati ya tarehe mbili tofauti katikati ya mwezi wa Juni.


Mwezi unaweza kuandama kati ya jioni ya Alhamisi ya Juni 14 au jioni ya Ijumaa ya Juni 15, kutegemeana na kuonekana kwa mwezi.


Kwa usahihi, ni kipindi gani waumini wamechagua kuonekana kwa mwezi hutofautiana kwa sababu wengine wamekubaliana mpaka wauone kwa macho huku wengine hata ukionekana kwingineko duniani sherehe hufanyika.


Kwa kuwa kuna siku 354 au 355 katika mwaka wa Kiislamu, siku ambayo Eid huangukia katika kalenda ya kawaida inayotumiwa duniani kote (Gregorian Calender) hubadilika kila mwaka.


Kwanini Waislamu husherehekea?


Waislamu hufunga kula kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanzia alfajiri mpaka kuzama kwa jua.


Ramadhani ni mojawapo ya nguzo tano za Uislamu - pamoja na Shahada ya Imani, Swalah, Kutoa Zakaah (kuwasaidia wenye dhiki) na Kuhiji Makkah - hivyo huwapatia Waislamu wasaa wa kutafakari juu ya maisha yao ya kiimani katika kuifuata Quran takatifu kama ilivyofunuliwa kwa Mtume Muhammad.


Kwahiyo, Eid ni sherehe ambazo huashiria kuisha kwa kipindi muhimu cha kiimani.


Waislamu husherehekeaje Eid?


Kwa kawaida, Eid husherehekewa kwa muda wa takribani siku tatu na ni siku ya mapumziko kwa mataifa ya Kiislamu na baadhi ya nchi nyingine duniani. Kwa Tanzania, husherehekewa kwa siku mbili ambapo wafanyakazi hawaendi kazini na wanafunzi hawaendi shuleni.


Kama zilivyo sherehe nyingine, watu husherehekea kwa namna tofauti, lakini kwa Waislamu huanza kwa kwenda mapema msikitini kuswali. Baada ya swalah kumalizika, waumini hutakiana heri ya Eid kwa kusalimiana, mara nyingi hukumbatiana mara tatu, wakati mwingine watoto hupewa zawadi kutoka kwa wakubwa wao.


Siku nzima iliyobakia hutumiwa kwa kusherehekea pamoja na familia na marafiki, kula na kupeana zawadi pamoja na kwenda kutembea sehemu tofauti. Familia nyingi hununua mavazi mapya kwa ajili ya kusherehea sikukuu hii.


Mara nyingi wakati wa sherehe za Eid huambatana na mapishi ya vyakula maalum ambavyo familia nyingi huwa hawavipiki siku za kawaida. Kwa Waislamu wengi huandaa biryani, pilau au wali, kwa nchini Tanzania, pilau ndiyo chakula maarufu kinachopikwa kwa nyama aidha ya ng’ombe, mbuzi, kuku, ngamia nakadhalika. 

Si jambo la kushangaza kipindi cha sherehe hizi kila mtaa utakaokatiza katika jiji la Dar es Salaam kunukia harufu ya pilau.       


Kuna tofauti gani kati ya Eid al-Fitr na Eid al-Adha?


Huwa kunakuwa na aina mbili za Eid kila mwaka. Ya pili, Eid al-Adha, husherehekewa baada ya miezi miwili na ni sherehe ambayo huja sanjari na Hijja, tukio la kiimani kwenda kuhiji Makka kila mwaka.


Hii inatarajiwa kusherehekewa kati ya Agosti 21 au Agosti 22 mwaka huu, hujulikana pia kama “sherehe ya kuchinja”, ikiwa ni heshima kwa kukumbuka tukio alilolifanya Mtume Ibrahim la kutaka kumtoa sadaka mwanaye wa kiume Ishmael, kitendo cha kutii amri ya Mwenyezi Mungu.


Unawezaje kumtakia mtu Eid njema?


Maneno maarufu ambayo hutumiwa na Waislamu ni “Eid Mubarak”, ambayo kwa Kiarabu yanamaaisha “Heri ya sikukuu ya Eid au Eid njema”


Hivyo basi watu wanaosherehekea sikukuu ya Eid husalimiana kwa mtindo huu kwa Click here to Reply or Forward

No comments: