Advertisements

Thursday, June 14, 2018

FUTARI MKOANI TABORA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) akisalimia na Sheikh wa Mkoa wa Tabora wa Ahamadiyya Musilim Jamaat Tanzania Shafi Mohamed Memon (kulia) jana mjini hapa wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi akitoa salamu za Waislamu wa Mkoa huu baada ya futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.
ya futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa dini na Serikali walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakifuatilia hotuba ya Sheikh wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi(hayupo katika picha) 
Baadhi ya Viongozi wa dini walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha)
Baadhi ya wageni kutoka madhehebu mbalimbali walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (hayupo katika picha) wakifuatilia hotuba yake.
Baadhi ya wageni kutoka madhehebu mbalimbali walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (hayupo katika picha) wakiaomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wa Mkoa wa Tabora.
Baadhi ya wageni kutoka madhehebu mbalimbali walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (hayupo katika picha) wakiaomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali na viongozi wa Mkoa wa Tabora.
Baadhi ya wageni kutoka madhehebu mbalimbali walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (hayupo katika picha) wakiaomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali na viongozi wa Mkoa wa Tabora.
Baadhi ya wageni kutoka madhehebu mbalimbali walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (hayupo katika picha) wakiaomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali na viongozi wa Mkoa wa Tabora.

HATUA YA VIONGOZI KUANDAA FUTARI NA KUWAALIKA WATU INAJENGA UMOJA –SHEIKH MAVUMBI
Na Tiganya Vincent- Tabora

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi amepongeza hatua ya viongozi mbalimbali wa umma na sekta binafsi kwa kuandaa futari kwa kuwa jambo linasaidia kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Aggrey Mwanri.

Alisema ni kweli Serikali haina dini lakini wananchi wanazo dini na hivyo hatua hiyo inaoonyesha mapenzi makubwa waliyonayo kwa watu wote bila kujali tofauti zao , hali inayosaidia kuimarisha umoja wa Kitaifa ulioasisiwa tangu uhuru wa Nchi ya Tanzania.

Sheikh Mavumbi aliwataka watu wengine ambao Mwenyezi Mungu amejalia kuwa na uwezo wa kifedha kuigia mfano ulionesha na baadhi ya viongozi wakiwemo wa Kitaifa wa kutoa futari kwa watu bila kujali rika na uwezo wao aua hali zao za kimaisha.

Aidha Sheikh huyo wa Mkoa aliwaomba umma wa kiislamu katika Mkoa wa Tabora endapo watafanikiwa kuuona mwezi muandamo kushiriki Swala ya eid El fitri itakayoswaliwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ikiwa ni baada ya kukamilika mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani.

Sheikh Mavumbi alisema  Baraza la Eid Kimkoa litafanyika katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tabora (Uhazili)

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri aliwashukuru Waislamu kwa nia yao njema ya kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika mapambano ya ukumbozi wa kiuchumi kwa wanyonge.

Alisema kuwa vita hiyo ni kubwa ni vema  Watanzania wote bila kujali tofauti za dini, kabila , vyama wakashikamana na kumuunga mkono Rais Magufuli ili hatimaye matunda ya vita hivyo yaweze kuwanufaisha watu wengi.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwaomba Viongozi wa Wawaislamu , Waumini na madhehebu mbalimbali kuhakikisha wanashirikiana na uongozi wa Mkoa wa Tabora katika mapambano ya matatizo mbalimbali yanayoukabili Mkoa huo ikiwemo utoro wa watoto mashuleni na mimba za utotoni.

Alisema lengo la Mkoa ni kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kuwa wawe shule tarehe Shule zitakapofunguliwa Mwezi ujao

Mwisho 

No comments: