Advertisements

Monday, June 11, 2018

HAUSIGELI AJINYONGA HADI KUFA, KISA WIVU WA MAPENZI

IKIWA zimebaki siku chache ili kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mrembo aliyejulikana kwa jina la Juliana Martin (miaka 23-25) Mkazi wa Mtaa wa Tushikamane Kata ya Lukobe nje kidogo ya Mji wa Morogoro, ambaye alikuwa akifanya kazi za ndani (house girl) amejinyonga hadi kufa huku chanzo cha uamuzi huo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Mrembo huyo anadaiwa kujifanyia ukatili huo usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita kwa kujitundika kamba juu ya mti kisha kujinyonga.

Juliana ambaye ni Mwenyeji wa Mkoa wa Dodoma Kijiji cha Magambua kabla ya kupatwa na umauti huo alikuwa akifanya kazi za ndani kwa familia ya Ustadh Mstaph Alude. Hata hivyo kwa watu waliokuwa wanashuhudia hakuna mtu aliyeweza kubaini kwa haraka chanzo cha kifo chake.

Akizungumza na Mwandishi wa www.globalpublishers.co.tz kwenye eneo la tukio, Mmoja wa majirani wa mrembo huyo ambaye alihusisha kifo hicho na wivu wa mapenzi. “ Huyu nasikia alikuwa na ugomvi na mwanaume wake sasa nasikia alipoachwa ndipo kamua kujinyonga” alisema jirani huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mwajuma Ally.

Wakizungumza na Mtandao huu mabosi wa Mrembo huyo Ustadh Aluke na Mkewe Rukia kwa pamoja walieleza tukio hilo mwanzo hadi mwisho.
“Jana jumamosi mida ya saa 2 usiku Juliana ambaye ni msichana wangu wa kazi niliyekaa naye kwa wema zaidi ya miaka 4 akaondoka hapa nyumbani na kurudi mida ya saa 4 huku akiwa na hasira nikaamua kuchukua simu yake nilipokagua nikakuta meseji za ugomvi akigombana na mpenzi wake.
Moja ya meseji hizo mwanaume huyo alimwambia kwamba nimemuacha mpenzi wangu kwa ajiri yako kisha wewe unanisaliti na Juliana akamjibu sijafanya hivyo hivi kile kivulana unachonihisi nacho nitakipeleka wapi?

“Meseji nyingine huyo mwanaume akamwita na kumtaka waachane kwa uchungu sasa tunahisi huenda ikawa chanzo cha yeye kuamua kujinyonga” alisema Rukia.
Kwa upande wake Ustadh Aluke alisema “Imeniuma sana huyu binti amekuja hapa kumlea mjukuu wangu tangu akiwa na miezi mitatu mpaka sasa ana umri wa miaka 4, tulikuwa tunaishi naye kama mtoto wetu ukweli alikuwa anatabia njema sana ila ndio hivyo tunahisi uhusiano wa kimapenzi huenda yamemsababisha kuchukua maamuzi hayo magumu”alisema Ustadh Akude na kuangua kilio kwa uchungu.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zilidai kwamba Polisi kwa kushirikiana na mabosi wa marehemu walichukua namba za simu kwenye simu ya Marehemu na kumpigia mwanaume huyo hakupokea licha ya kupigiwa zaidi ya mara tatu.
Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Octavian Joseph alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake.

Na Shekidele, Morogoro.
MEMORISE RICHARD.

GPL

No comments: