ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 11, 2018

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA WFP NCHINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Bw. Michael Dunford alipofika Wizarani kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu unaofanywa na Shirika hilo hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Mwakilishi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa anaopata katika kutekeleza majukumu yake. Shirika la WFP hapa nchini linajishughulisha katika kusaidia miradi mbalimbali ya kilimo katika kuwajengea uwezo wakulima wadogo, lishe na kusaidia upatikanaji wa soko kwa wakulima wadogo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimatifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy kwa pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Bw. Dunford hawapo pichani 
Bw. Dunford akifafanua jambo kwa Prof. Mkenda wakati wa mazungumzo yao 
Mazungumzo yakiendelea 
Prof. Mkenda akiagana na Bw. Dunford mara baada ya mazungumzo kati yao

No comments: