Hivi karibuni, sensei Fundi Rumadha, Dan 4( Yondan), alipata firsa yenye hadhi kubwa kuchaguliwa kufanya mahojiano na gazeti maarufu la visiwa vya Okinawa, "OKINAWA TIMES".Visiwani Okinawa, ndipo chimbuko halisi la asili na mwanzo wa sanaa ya Karate ilipozaliwa duniani. Ni adimu sana kuona kwamba sehemu ilipozaliwa au kubuniwa michezo ya Karate kuwa na shauku ya kutaka kujua nini hasa maendeleo ya Karate kwa nchi kama Tanzania ambayo haina hata kiwango cha kueleweka kimafunzo, licha ya Karate kuwa hapa kwa karibu miaka 50 sasa, pasipo hata msaada wa kumbi za mazoezi ikiwemo changa moto kubwa mno miaka nenda , miaka rudi na isiyoeleweka kulinganisha na nchi za jiranihapa Afrika mashariki na ya kati. Kifupi tu
nawezasema,hii ni bahati sana kwa jina la nchi yetu ya Tanzania na umaarufu wake wa utalii ndipo hapo watu wa Japan, waliona je, kuna sanaa yao ya michezo asilia ya Karate Tanzania? Ilinipa faraja sana kwa mahojiano ya mfumo wa Karate wenye chimbuko lake huko Okinawa, uitwao, Okinawa Goju Ryu, au kwa maana nyingine, mtindo maarufu wa Karate toka Okinawa.
Pia, napaenda tu kwa wale wana Karate wa Tanzania, hususani mtindo wa Goju Ryu kujua kwamba sio lahisi kwa jinsi Masters wa Karate na walimu wakubwa wote wapo huko Okinaw, lakini waliona bora tu kuichagua Tanzania na kujua lipi linaloendelea baada ya sensei Fundi Rumadha kuwapandisha ngazi baadhi ya walimu na wanafunzi wa chama cha Jundokan Karate miezi michache iliyopita.
Pia vilevile, sensei Fundi Rumadha, ameshakubali mwaliko wakurudi tena visiwani humo mwezi Novemba 8 hadi 16 kuadhimisha miaka 65 ya toka chama cha Jundokan kilipoanzaniashe na mwalimu Master Eiichi Miyazato, ambaye pia ni aliuwa ni mwalimu wa sensei Nantambu Camara Bomani, mwanzilishi wa tawi hilo hapa Tanzania. Kongamano hilo litahudhuriwa na masensei wote wa Okinawa Goju Ryu duniani, litalifanyika mjini Naha, Okinawa katika sehemu muhimu sana iitwayo "Okinawa Budokan".
Kutakuwa na maonyesho ya Karate, semina za jinsi ya utumiaji mbinu za Karate, na kutembelea makumbusho ya Karate na pia makaburi ya wa asisi wote wa Karate wa Okinawa.Hii ni moja ya maadhimisho ambayo hufanyika kila baada ya miaka mitano, na sio kila mwaka, kufuatana na usemi wa mwenyekiti wa chama hicho, pia mtoto wake na master Eiichi Miyazato aitwae Kancho, Yoshihiro Miyazato mwenye umri wa miaka 65 alizaliwa sawa na muda ambao baba yake ndipo alianzisha chama hicho.


No comments:
Post a Comment