ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 12, 2018

MKUU WA MAJESHI ATOA WITO KWA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU

 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa, iliyofanyika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka akionesha sehemu ya fedha alizochangia katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akikabidhi  sehemu ya fedha zilizochangwa na Kamti ya Ulinzi na Usalama na Wafanyabiashara wa Mkoa huo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani humo.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiongoza Kwaya ya Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa ejngo la  Kanisa, iliyofanyika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, (wa pili kushoto) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka akicheza pamoja na wanakwaya.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye kipaza sauti) akikabidhi  sehemu ya fedha zilizochangwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wafanyabiashara wa Mkoa huo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani humo.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbele ya jiwe la msingi la Ujenzi wa Kanisa Parokia ya Ilumya, baada ya harambee ya kuchangia ujenzi wa ejngo la  Kanisa, iliyofanyika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, (katikati) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
 Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya yaBusega, Mhe. Tano Mwera katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani humo.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo(wa nne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya, (wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo(wa nne kushoto) na baadhi ya viongozi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya, (wa pili kushoto) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo(wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Busega na Bariadi.

Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo ametoa wito  kwa wazazi kuwekeza katika elimu kwa watoto  wao ili waweze kutimiza ndoto za maisha yao, badala ya kuwaoza wakiwa na umri mdogo.

 Jenerali Mabeyo ametoa  wito huo wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya  iliyofanyika Kijiji cha Masanza Kona  kata ya Kiloleli Wilayani Busega, na kuhudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Vicent Naano  marafiki wa mkuu wa majeshi kutoka Dar es Salaam , Wajenzi Enterprises ,wafanyabiashara wa Simiyu na waumini wa kanisa hilo .

Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo pamoja na kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa amesema pamoja na jamii kushiriki katika ujenzi wa nyumba za ibada ,wazazi wanapaswa kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto badala ya kuwakatisha masomo hususani  wa kike ili waolewe .

“Sasa hivi mmewekewa shule ya sekondari hapa na mimi nimeshiriki kujenga shule hii DC analijua hili, sasa wazee wangu mlioko hapa changamkieni elimu, watoto muwapeleke shule, waacheni wasome elimu ndiyo ufunguo wa maisha, wasiposoma hata mkiomba nafasi za kuingia jeshini hakuna nafasi” alisema Jenerali Mabeyo

Wakizungumza  kwa niaba ya Waumini wa Parokia ya Ilumya Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga na Padri Kizito Victor na  Paroko wa Parokia ya Masanza Padri Michael Gumalija wameshukuru  Mkuu wa Majeshi na Viongozi na wadau wengine wote waliochangia na kuahidi kushirikiana na wafadhili wote kuhakikisha kanisa linajengwa.

Katika hatua nyingine Jenerali Mabeyo ameahidi kuchangia Ujenzi wa zahanati bora itakayowekwa vifaa vya kisasa vyenye hadhi ya Hospitali katika Kijiji cha Masanza na kuwahakikishia waumini kuwa mara baada ya kukamilika kwa jengo la kanisa, ujenzi wa zahanati hiyo utaanza mara moja.  

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema  kipaumbele cha kwanza cha Mkoa wa Simiyu ni elimu, hivyo Mkuu wa Majeshi amesaidia kufikisha ujumbe wa kuhamasisha elimu kwa wazazi, jambo ambalo limekuwa sehemu ya kampeni ya mkoa ya kupinga mimba za utotoni ambazo zinaua ndoto za watoto wa kike.

“Sisi tunaona Mkuu wa Majeshi ametusaidia kwenye kampeni ya mtoto wa kike na tatizo la mimba ambalo linaua ndoto za watoto wa kike na sisi kama mkoa wakati wote tumekuwa tukiwaambia mimba za utotoni zinaua ndoto zao utotoni, maneno haya ameyasema Mzee Mabala na mimi naona ni kauli mbiu nzuri kwa wazazi dhidi ya watoto wao wa kike” alisema Mtaka.


Katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya lumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo jumla ya fedha zilizopatikana ahadi na taslimu ni shilingi 273,135,850/=kati ya hizo  fedha taslimu shilingi 111,965, 850/= , ambapo zinahitajika jumla ya shilingi milioni 782 kwa ajili ya kukamilisha kujenga jengo lenye uwezo wa kuchukua waumini zaidi ya 1200 kwa mara moja

No comments: