Advertisements

Friday, June 22, 2018

Sami Hyypia asisitiza kujituma kufanikiwa

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) akizungumza kwenye hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kulia).
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza na timu (hazipo pichani) zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ gwiji huyo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (kushoto) na Meneja Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered nchini, Mariam Sezinga wakipitia ratiba ya hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani).
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia wakikabidhi vifaa vya michezo kwa Afisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Mubaraka Kibarabara (katikati) ambapo Airtel ni moja kati ya washiriki 32 wa mashindano ya ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki kutoka kampuni mbalimbali wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (hayupo pichani) wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaa. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani).
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akisaini ‘Autograph’ kwa baadhi ya timu zitakazoshiriki mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akisalimiana na baadhi ya timu kutoka makampuni mbalimbali zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia katika picha ya pamoja na timu kutoka makampuni mbalimbali zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia katika picha ya pamoja na timu ya waandishi wa habari watakaoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia wakikabidhi vifaa vya michezo kwa makapteni wa kampuni mbalimbali zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia kwa pamoja wakimkabidhi vifaa vya michezo kapteni wa timu ya waandishi wa habari Bw. Majuto Omary wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd. wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Sami Hyypia veterani wa timu ya Liverpool ambaye yupo nchini kwa mwaliko wa benki ya Standard Chartered amesema kuwa mwanasoka wa mafanikio kunahitaji kazi ngumu na kujituma.


Alisema tangu utoto wake amekuwa akijituma na anaamini katika kujituma katika shughuli zinazokuinua.


Alisema hayo katika hafla ya kukabidhiana vifaa kwa timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la Standard Chartered inayotarajiwa kufanyika jumamosi wiki hii, iliofanyika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.


Alisema kwamba kuwa juu katika soko kunatokana na mambo mawili makubwa ambayo ni kujituma na kuwa na kipaji.


Alisema hata ukiwa na kipaji ukibweteka katika mazoezi na kujituma katika kuhakikisha uko fiti katika maisha ya mwanasoka huwezi kufikia ngazi za juu za uchezaji wenye kuheshimika.


Alisema pamoja na kuja kuangalia michuano hiyo amepata nafasi ya kuzungumza haja ya kukua katika soka kwa kutengeneza nidhamu inayotakiwa ya kujituma, kufanya mazoezi na kutumia kipaji katika kuimarisha usakataji soka.


Alisema kwamba amebaini kuwepo kwa vipaji vingi nchini Tanzania kinachotakiwa ni kuendelezwa kwake na pia wenye vipaji kujituma kwa nguvu ili kutekeleza ndoto zao.


Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank nchini Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, alisema benki yake imekuwa na uhusiano na klabu ya Liverpool kwa muda mrefu na kwamba wameingia mkataba utakaomalizika mwaka 2023.


Alisema umuhimu wa ushirikiano wao ni ile hali ya kuongeza thamani katika usakataji wa soka, kuleta ujirani na urafiki miongoni mwa wapenzi wa soka na kuanzisha kwa mahusiano ya kirafiki.


Aliwataka washiriki ambapo kila timu ina watu saba kutengeneza uwezo mkubwa wa ushindi ili waweze kwenda katika tripu ya siku 3 nchini Uingereza.


Michuano ya soka ya Standard Chartered hufanyika kwa kila mchezo kutumia dakika 10.


Michuano hii ya tatu nchini Tanzania toka ianzishwe mwaka 2005 itashirikisha timu 32 zinazotokana pia na wateja wa benki hiyo.

No comments: