Picha zilizopigwa wakati wa mkutano zinaonyesha Trump na Kim wakitia saini nyaraka ikiwa ni ishara kwamba viongozi hao wamekubaliana “kufanyia kazi mpango wa kuondokana na silaha za nyuklia katika Rasi ya Korea.”
Katika makubaliano hayo, Trump amekubali "kubeba dhamana ya usalama" wa Korea Kaskazini.
Nyaraka hizo walizotia saini pia zinaonyesha kwamba viongozi hao watajibidiisha kuanzisha “uhusiano mpya kati ya Marekani na DPRK (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Watu wa Korea)”
"Nafikiri uhusiano wetu kwa ujumla na Korea Kaskazini na Rasi ya Korea utakuwa katika hali tofauti sana kuliko ilivyokuwa awali," alisema Trump alipokuwa akihitimisha mazungumzo yao yaliyomalizika kwa hafla ya utiaji saini.
"Leo, tulikuwa na mkutano wa kihistoria na tumeamua kuachana na yote yaliyopita,” Kim alisema kupitia kwa mkalimani wake. "Dunia itashuhudia mabadiliko makubwa." Mwanachi
No comments:
Post a Comment