Advertisements

Friday, June 22, 2018

WANAMUZIKI NCHINI KUTEMBELEA BUNGE WIKI IJAYO KUPITIA TAMUFO

Rais  wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tamufo, Morocco Dar es Salaam jana wakati wa  kujadili masuala mbalimbali ya umoja huo pamoja na safari ya baadhi ya wanachama wa Tamufo kwenda Bungeni Dodoma.
Mhandisi Abdallah Ally kutoka  Kampuni ya CogsNet ambayo inasimia kazi za wasanii akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.
Rais  wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akiteta jambo na Katibu wa umoja huo, Stellah Joel wakati wa mkutano huo.
Msemaji wa Kampuni ya CogsNet ambayo inasimia kazi za wasanii, Ahmed Kipozi  akizungumza kwenye mkutano huo
Mwanamuziki Hamza Kalala akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kiki.
Katibu wa umoja Tamufo, Stellah Joel, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Mwanamuzi mahiri Kitenzogu Makassy, akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwanamuziki Hamza Kalala.
Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kiki akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Witness Kibonge, akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Stellah Joel, akizungumza kwenye mkutano wa kujadili safari hiyo ya Bungeni Dodoma.
Wanamuziki Hamza Kalala na Mzee Makassy wakiteta jambo kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

WANAMUZI walio wanachama wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO) wiki ijayo watatembelea Bunge kwa ajili ya kuona mambo mbalimbali yanayofanyika ndani ya Bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa Umoja huo, Dk.Donald Kisanga alisema kwa umoja huo kwao ni fursa kubwa ya kutembelea Bunge.

"Kwetu sisi Tamufo kutembelea Bunge ni fursa kubwa na tunaenda kuona jinsi Bunge linavyofanya kazi yake" alisema Kisanga.

Kisanga alisema msafara wao utaondoka jijini Dar es Salaam Juni 23 na Bungeni watakuwepo Juni 25 mwaka huu na mwenyeji wao ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harrison Mwakyembe.

Kisanga aliyataja baadhi ya makundi ya wanamuziki watakaokuwepo kwenye msafara huo kuwa ni wanamuziki wa dansi ambalo litaongozwa na Mwanamuziki mkongwe Boniface 
Kikumbi Mwanza Mpango au King Kik na Hamza Kalala.

Alitaja kundi la muziki wa Injili kuwa litaongozwa na Stella Joel na Emanuel Mbasha wakati Bongo Fleva litaongozwa na Witness Kibonge Mwepesi huko taarabu likiongozwa na Sizer Masogelo na Muziki wa Asili likiongozwa na  Grace Kayinga.

Katibu wa Tamufo, Stellah Joel alisema wanamuziki kutoka mikoa yote waliotayari watakuwepo kwenye msafara huo.

No comments: