Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam
Omary, (kushoto), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa
waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya
viwango hatarishi mahala pa kazi.
Na
mwandishi wetu, Tanga Juni 21, 2018
WAAJIRI wanao wajibu wa
kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wao unapewa umuhimu wa kwanza na moja ya
njia ya kutekelza hilo ni kufanya tathmni ya viwango hatarishi mara kwa mara.
Hayo yamesemwa leo Juni
21, 2018 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Thathmini wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, wakati akifungua mafunzo ya siku
moja kwa waajiri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri katika kuhakikisha
usalama na afya ya mfanyakazi unazingatiwa.
Lakini pia aliwataka
wafanyakazi nao watekeleza wajibu wao kwa kutumia vifaa kinga walivyopewa na
waajiri wao pale wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi ili kupunguza ajali
zinazoweza kuzuilika.
Alisema ili kutekeleza
awajibu huo wa kisheria, wajiri wanapaswa kufanya tathmini ya mara kwa mara ili
kubaini vihatarishi mahala pa kazi ili kuchukua hatua ya kuzuia majanga
yatokanayo na kazi.
“Ifahamike
kuwa sisi WCF wajibu wetu wa msingi ni kulipa fidia stahiki na kwa wakati kwa
mfanyakzi aliyeumia, kuugua au kufariki wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi,
ikiwa ni pamoja na kusajili na kupokea michango kutoka kwa waajiri walio katika
sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara, lakini pia tunalo jukumu la kisheria la
kukuza mbinu za kuzuia ajali na vifo kazini kwa kutoa elimu kwa waajiri lakini
pia wafanyakazi wenyewe na hiki ndicho tunachokifanya hapa leo.” Alisema
Dkt. Omary amabaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba.
Katika kuhakikisha
wadau wanapata uelewa wa kutosha kuhusu majukumu ya Mfuko na wajibu wao katika
kutekeleza sheria iliyoanzisha Mfuko, tumekuwa tukikutana na waajiri na kuwapa
elimu kupitia semina kama hii ya leo, lakini pia tumekuwa tukitembelea maeneo
ya kazi na kwa kushirikiana na waajiri wenyewe tumekuwa tukitoa elimu kwa
wafanyakazi pia, alisema Mkurugenzi huyo wa hudumaz a Tiba na Tathmini.
“Na kwa hakika
kumekuwepo na kukua kwa uelewa miongoni mwa waajiri, kuhusu shughuli za Mfuko,
awali waajiri walidhani Mfuko kazi yake ni kusajili na kukusanya michango tu,
lakini kupitia elimu hii tunayotoa kuhusu shughuli za Mfuko, kumekuwepo na
mabadiliko makubwa, tumekuwa tukipokea maombi mengi kutoka kwa waajiri wakitaka
tutembelee maeneo yao ya kazi, ili kutoa elimu hii kwa wafanyakazi pia, jambo
ambalo hapo awaali wakati tunaanza halikuwepo na hakika kwetu sisi haya ni
mafanikio.”
Dkt. Omary alisema, kwa
sasa Mfuko umekuwa ukitekeleza majukumu yake kwa mafanikio makubwa ambapo zaidi
ya waajiri 14,224 wamesajiliwa na wengine wapya wanaendelea kujisajili.
Mafaniukio mengine
yaliyopatikana katika kipoindi kifupi, Mfuko umeweza kutekeleza jukumu lake la
msingi la kulipa fidia satahiki na kwa wakati kwa wafanyakazi walioumia, kuugua
au kufariki kutokana na kazi kwa mafanikio makubwa.
“Pamoja na uchanga
wake, Mfuko umeshalipa fidia kiasi cha
shilingi bilioni 2.52 kwa wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na
kazi, haya ni mafanikio makubwa ambayo Mfuko umeyapata katika kipindi kifupi”.
Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) ni taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa kwa mujibu
kifungu namba 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura ya 263 iliyofanyiwa
marejeo mwaka 2015, lengo kuu likiwa ni kulipa fidia stahiki na kwa wakati
lakini pia kusajili na kukusanya michango kutoka kwa waajiri walio katika sekta
ya umma na binafsi Tanzania Bara.
Mfuko ulianzishwa mnamo
mwaka 2015 na Serikali ilitoa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja ili kujiweka
sawa na ilipofika Julai 2016 tulianza kupokea madai ya fidia.
Washiriki wakiendelea kuchukua nafasi zao.
Baadhi ya washiriki wakisoma majarida ya WCF yenye maelezo mbalimbali kuhusu shughuli za Mfuko.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa WCF, Bi. Laura Kunenge, (katikati), Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi (kushoto) na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine wakipitia taarifa mwanzoni mwa mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa WCF, Bi. Laura Kunenge, akiongoza mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam
Omary, (kulia aliyesimama), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa
waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya
viwango hatarishi mahala pa kazi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam
Omary, (kushoto aliyesimama), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa
waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya
viwango hatarishi mahala pa kazi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam
Omary, (kulia aliyesimama), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa
waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya
viwango hatarishi mahala pa kazi. wengine pichani meza meza kuu ni, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi (kushoto) na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine
Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine, akizungumza.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
Picha ya kwzna ya pamoja.
Picha ya pamoja ya pili. |
Mshiriki akijiandikisha. |
No comments:
Post a Comment