Wakati siku zinakaribia na matayarisho yamekamilika kwa kuanza maonyesho ya kimataifa ya Intern.Afrika Festival Tubingen 2018 yanayo ambatana na maonyesho ya biashara ya (GaiExpo) German-Afrika International Expo,kuanzia tarehe 9 Agosti 2018 mpaka 12 Agosti 2018 katika mji wa Tubingen,nchini ujerumani ambapo nchi lengwa katika maonyesho hayo mwaka 2018 ni TANZANIA. baadhi ya wasanii na bendi mbali mbali wameshathibitisha kushiriki katika maonyesho hayo kati ya bendi za muziki wa dansi maarufu kama "Bongo Dansi" zilizokuwa tayari huko ulaya ni bendi maarufu za Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni au "Viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens " yenye makao yake ujerumani, pia kuna Saidi Kanda na Mvula-Mandondo Band inayoongozwa na mwanamuziki Saidi kanda yenye makao yake kule Uingereza nao wameshakuwapo tayari tayari kwa kutumbuiza katika maonyesho hayo makubwa. Watayarishaji wa maonyesho hayo GaiExpo wamesema wanatarajia kupokea wageni wengi kutoka nchini Tanzania wakiwemo wafanyibiashara,wajasilimali,wasanii n.k,mialiko imeshatumwa kwa wageni wote na pia kopi za mialiko hiyo zimeshatumwa kwa ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania kilichobakia ni jukumu la ubalozi wa ujerumani uwape idhini na viza za kusafiria washiriki wa maonyesho hayo makubwa ambayo kwa mara ya kwanza Tanzania ni nche lengwa katika tamasha kubwa barani ulaya. http://afrikafestival.net/
http://gabs-germany.com/gaiexpo
info@gabs-germany.de
kontakt@afrikafestival.net
No comments:
Post a Comment