Advertisements

Monday, July 16, 2018

BILIONI 1.5 KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO

 Meneja wa Wakala wa Majengo nchini(TBA) Mkoa wa Simiyu Mhandisi Likimaitare Naunga (wa pili kulia) akimuonesha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(katikati) ramani ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, mara baada ya Waziri Ummy kutembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali hiyo Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akimuongoza  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Ummy Mwalimu , wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni  wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
 Waziri wa afya jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu sambamba na kaimu mkurugenzi wa Amref helth Africa Dr Aisa Mmmuya kulia akishuhudia tukio hilo la uzinduzi huo.
Waziri wa afya Ummy Mwalimu sambamba na mbunge wa Itilima Njalu Silanga wakielekea kuzindua mradi wa tuwatumikie.
                                (PICHA ZOTE NA SHUSHU JOEL)

Na Shushu Joel, Bariadi
Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu Jana mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje(OPD)  la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, ambapo ameridhishwa na ujenzi wa jengo hilo.

Waziri Ummy amewahakikishia viongozi wa mkoa wa Simiyu kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.5 na wadau wengine wameahidi kutoa shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha wodi ya mama na mtoto mkoani humo ili kupunguza hadha ya kuwachanganya watoto na wakubwa kipindi wanapokwenda kupata matibabu.

“Simiyu katika bajeti ya Serikali imetengewa shilingi bilioni 1.5 lakini tumepata pia shilingi bilioni 1.1 kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya ujenzi waWodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, lengo letu ni kukamilisha ujenzi haraka ili tuiwezeshe Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kuchukua majengo ambayo yanatumika sasa hivi kama Hospitali Teule ya mkoa” alisema Ummy.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy alisema baada ya kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Serikali ina mpango wa kujenga Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Mashariki Mkoani Simiyu, itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga  ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambayo inahudumia mikoa takribani minane.

Aidha  pamoja na kuwa na mpango wa kujenga Hospitali ya hiyo Rufaa ya Kanda Simiyu, Serikali imekusudia kujenga Hospitali za Kanda tatu ambazo ni Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambayo imeanza kujengwa Mtwara, nyingine itajengwa Tabora(Kanda ya Magharibi ili wananchi wapate matibabu ya kibingwa katika maeneo yao.

Pamoja na Serikali kuahidi kutoa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa SIMIYU,  pia Waziri Ummy amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali yaWilaya ya Itilima.

Naye mkuu wa Mkoa wa Simiyu  Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kujenga jengo hilo, ambazo zitasaidia kuboresha huduma za afya katika mkoa wa Simiyu kwa


Aidha, Mtaka alisema kuwa ardhi kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Mashariki itatolewa bure na akamhakikishia Waziri Ummy ushirikiano wa asilimia 100 kila watakapokuwa wakihitajika kwa namna moja au nyingine ili kufanikisha ujenzi wa hospitali hiyo.

No comments: