Advertisements

Friday, July 13, 2018

JICHO LA VIJIMAMBOBLOG UWANJA WA NDEGE WA DAR-ES-SALAAM VISA PROCESS

Utaratibu wa utoaji visa kwa wageni wanaoingia Tanzania kupitia airport ni kero na usumbufu kwa wageni, Unapita dirishani unatoa passport yako na kufanyiwa alama ya vidole kisha unaenda kulipia visa dirisha lingine na kuambiwa usubiri zaidi ya saa moja visa yako kushughurikiwa ni usumbufu kwa wageni na aibu kwa nchi na wizara ya mambo ya ndani. Baada ya visa kukamilika officer wa uhamiaji anaita mgeni mmoja mmoja kumkabizi passport yake hii inatengeneza mazingira ya rushwa. Na pia ukosefu wa uduma ya wifi uwanjani ni usumbufu mwingine kwa wageni kwani hata kama una dharura uwezi kuwa na mawasiliano wizara ya mambo ya ndani ifanyie kazi mapungufu haya. 

Wageni wakisubiri passport zao zikishughurikiwa kugongwa visa.

Ukiwa umechukua body spray hata kama ni zawaidi jiandae kulipia ushuru usiokuwa na receipt.

1 comment:

Anonymous said...

Sioni ubaya wa kusubiri. Ni kwa ajili ya usalama wa Taifa (National security) kuhakikisha visa zinatolewa kwa wale wanaostahili. Kumbuka mdau, huku ughaibuni tunakaa airport nyakati nyingine zaidi ya saa tatu tunaposafiri, lengo likiwa ni usalama. Hivyo basi, maoni yako mdau yanapotosha kidogo.