Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Suzan Mlawi (Katikati) akizungumza na timu ya Kilimanjaro Queens (haipo pichani) baada ya kurejea nchini ikitokea Rwanda kwenye mashindano ya ligi ya Wanawake ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati ambapo imefanikiwa kutetea ubingwa wa michuano hiyo.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo Bw.Orest Mushi na kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF Bw.Kidao Wilfred.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Suzan Mlawi (Katikati) akipokea Kombe kutoka kwa Nahodha wa Timu ya Kilimanjaro Queens Bi Asha Rashid baada ya kurejea nchini ikitokea Rwanda kwenye mashindano ya ligi ya Wanawake ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati ambapo imefanikiwa kutetea ubingwa wa michuano hiyo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo akizungumza na Timu ya Kilimanjaro Queens (hawapo katika picha) baada ya kurejea nchini ikitokea Rwanda kwenye mashindano ya ligi ya wanawake ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati ambapo imefanikiwa kutetea ubingwa wa michuano hiyo.
Nahodha wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu “Kilimanjaro Queens”Bi Asha Rashid akizungumza wakati timu hiyo ilipopokelewa leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Suzan Mlawi ikitokea Rwanda kwenye mashindano ya ligi ya wanawake ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati ambapo imefanikiwa kutetea ubingwa wa michuano hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Suzan Mlawi (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya mpira wa Miguu ya wanawake “Kilimanjaro Queens” na viongozi wengine baada ya kuipokea timu hiyo iliyotokea nchini Rwanda kwenye mashindano ya ligi ya wanawake ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati ambapo imefanikiwa kutetea ubingwa wa michuano hiyo.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake “Kilimanjaro Queens” imerejea nchini ikitokea Rwanda ilipokuwa ikishiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA ambapo imefanikiwa kutwaa Kombe la michuano hiyo.
Timu hiyo imepokelewa leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Suzan Mlawi ambaye mbali tu na kuipongeza timu hiyo lakini pia ameishukuru kwa kuipeperusha vyema Bendera ya nchi.
“Mmeiwakilisha vizuri nchi yetu mmeonyesha nidhamu na kubwa zaidi mmeshinda na kufanikiwa kutetea kombe lenu nawapongeza sana na nawaahidi Serikali itaendelea kushirikiana na nyie ili mlete mafanikio zaidi kwa nchi yetu”Alisema Bibi Suzan.
Aidha Bibi Suzan amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF ) kutafuta mikakati mizuri itakayosaidia timu hiyo kupata wadhamini kama zilivyo timu nyingine lakini pia kuandaa tuzo kwa wachezaji wanaofanya vizuri ili kutoa hamasa kwa wadau wengi kutoa ushirikiano wa kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Bw. Kidao Wilfred ameeleza kuwa mafanikio waliyopata Kilimanjaro Queens yametokana na ushirikiano mkubwa baina ya Serikali Jeshi la Kujenga Taifa, Benchi la ufundi pamoja na Taasisi yake kwa kuwa karibu, kuijenga na kuiandaa timu hiyo vizuri.
Naye kocha wa timu Bw.Bakari Shime amesema kuwa timu yake imefanya vizuri kutokana na kufuata maelekezo mazuri aliyowapa na wakayafuata, timu kucheza kwa weledi mkubwa pamoja na ushirikiano mzuri kwa wadau wa mpira wa miguu kwa wanawake.
“Vijana wamejituma sana wamekuwa na ari ya kutetea Kombe hili na kuhakikisha wanarudi nalo nyumbani na imekuwa hivyo,wamekuwa na nidhamu na wamesikiliza maelekezo tuliyowapa”Alisema Kocha Bakari Shime.
Timu ya Kilimanjaro Queens imetwaa ubingwa wa michuano ya Afrika Mashariki na Kati baada ya kuichapa Ethiopia magoli manne kwa moja na ndio timu iliyoshinda magoli mengi katika michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment