JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri Mkuu wa Jamhu TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Bw. David M. Baesley atafanya ziara ya kikazi nchini kuanzia tarehe 25 Julai 2018 hadi tarehe 03 Agosti 2018. Ziara hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na WFP.
Wakati wa ziara hiyo nchini, Bw. Baesley ataonana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kitaifa kwa lengo la kujadiliana nao kuhusu maeneo ya ushirikiano kati ya WFP na wakulima wadogo kupitia mpango wa “Social Protection Programmes”; Mfumo wa Serikali wa Usalama wa Chakula; na masuala ya Wakimbizi na Jamii zinazozunguka hifadhi za wakimbizi pamoja na njia za kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Bw. Baesley anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 25 Julai, 2018 kwa ajili ya kuanza ziara hiyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dodoma.
24 Julai 2018
No comments:
Post a Comment