Advertisements

Tuesday, July 10, 2018

MTANANGE WA SIMBA NA YANGA UGHAIBUNI, SIMBA YAIFUNGA YANGA KWA MATUTA

Na Mwandishi wa Vijimambo Blog, Washington, DC
Mechi ya Simba na Yanga ambayo ni sehemu ya Old School Reunion iliyochezwa siku ya Jumamosi July 7, 2018 Washington, DC na kuishia 1-1 na mshindi Simba kuibuka kwa mikwaju ya penati.

Mechi hiyo iliandika historia nyingine baada ya Star wa bongo Movie Monalisa kuwepo uwanjani kushuhudia mapambano hu.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na refa wa FIFA aliyekuja maalum toka Tanzania Kazi Kipenga ambaye pia ni mfanyakazi wa Azam TV kwenye kipindi chake cha Kipenga.

Mpaka mapumziko timu zote zilikua hazinjafungana, mpambano huo umeweka historia kwa timu zote kucheza kandanda safi lililojaa kila aina ya ufundi.

Kipindi cha pili Simba ndio ilikua yakwanza kupata bao baada ya mchezaji wao Yusf kukwatuliwa ndani ya eneo la hatari na refa kuamuru ipigwe penati,

Baada ya bao hilo Yanga ililishambulia goli la Simba kama nyati aliyejeruhiwa na kunako dakika ya 85 Yanga ilisawazisha goli kwa bao safi lililofungwa na mchzaji Dullah Makubely.

Baada ya dakoka 90 mechi iliisha kwa timu zote kufungana bao 1-1 na ndipi zilipigiana penati tano, tano na timu zote kupata penati 3 na kukosa 2 ndipo zikaenda kupigwa penati moja,moja na Yanga kukosa yao wakati wenzao Simba kufunga yao na wao kuibuka washindi kwa jumla ya maao 5-4 dhidi ya Yanga.
 Timu ya Yanga

Timu ya Simba
Wachezaji wakisalimiana
Wachezaji wakisalimiana
 Yanga ikipasha misuli kabla ya mechi
 Simba wakipasha kabla ya mtanange
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

 Yanga wakipata mawaidha wakati wa mapumziko
Simba wakipata mawili matatu wakati wa mapumziko
 Mully na wanae
 Hadji na God
Bongo Movie star Monalisa watano toka kushoto akishuhudunia mpambano wa Yanga na Simba ughaibuni

Mashabiki wakifuatilia mpira
Mashabiki wakiwa uwanjani
Bongo movie Monalisa wa tano toka kushoto akifuatilia mpambano wa Simba na Yanga
Mashabiki mbalimbali wakiwa uwanjani
Mashabiki
Wapenzi wa mpira wakifuatilia
Ukodak moment
Kushoto ni Missy Temeke na Miss Kigoma wakishuhudia matanage
Monalisa Bongo Movie Star akifanyiwa mahojiano na Azam TV
wakati wa penati


No comments: