ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 28, 2018

Rais Magufuli awateua ‘wapinzani’ nafasi za Ukuu wa wilaya

By Mwandishi Wetu, Mwananchi. mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa, wa wilaya na makatibu tawala nchini huku akiwateua wanasiasa watatu waliowahi kuwa vyama vya upinzani katika nafasi hizo.

Akitangaza mabadiliko hayo leo Julai 28, Rais Magufuli amemteua David Kafulila kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.

Kafulila aliwahi kuwa mbunge wa NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia CCM.

Pia amemteua Moses Machali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Machali aliwahi mbunge wa Kasulu Mjini, (NCCR-Mageuzi) kabla ya kuhamia ACT-Wazalendo na baadaye CCM.

Kadhalika Rais Magufuli amemteua Patrobas Katambi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma. Katambi alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema.







No comments: