RC MAKONDA AMALIZA MIGOGORO SUGU ILIYOWATESA WAKAZI WA TABATA LIWITI*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo ametegua kitendawili kilichowatesa kwa muda mrefu wakazi wa *Kata ya Liwiti* baada ya mmoja wa wananchi kudai ndie *mmilika* halali wa *eneo la Soko* lao jambo lililotaka kupelekea *uvunjifu wa Amani*.
Akizungumza kwenye *Mkutano wa hadhara* na wananchi hao *RC Makonda* ameagiza *eneo hilo kurejeshwa kwa wananchi* kwaajili ya matumizi ya *Soko* baada ya kubainika kuwa anaedai eneo hilo aliuziwa kihalali alijichanganya badala ya kwenda *kiwanja kilichopo Block No. 200A kujikuta anakwenda Block No. 200B* ambacho kwa mujibu wa Ramani ya Mipango miji ni *eneo la Umma.*
Kutokana na Mkanganyiko huo *RC Makonda* ameagiza Mama huyo kuonyeshwa kiwanja chake *Block No. 200A* na kuagiza *asitokee mtu yoyote wa kuwabugudhi wananchi* na eneo lao la soko.
Aidha *RC Makonda* ameagiza *kuvunjwa Mara moja kwa ukuta* mmoja wa mwananchi aliejenga kwenye *eneo la hifadhi ya barabara* na kusababisha *usumbufu* kwa wakazi wa mtaa wa Amani Kata ya *Tabata Liwiti* kukosa sehemu ya kupita na kujikuta wanazunguka *umbali mrefu.*
Pamoja na hayo *RC Makonda* pia ameagiza *Uwanja wa mpira wa Tabata Sigara* kurejeshwa kwa wananchi kwaajili ya *matumizi ya michezo* baada ya wananchi kulalamika kuwa alienunua *Magorofa ya Sigara* anadai kuwa amenunua pia *eneo la Kiwanja* na kusababisha kukosekana kwa eneo la michezo.
Sambamba na hayo *RC Makonda* amempongeza *Mbunge wa Jimbo la Segerea Mhe. Bona Kalua* kwa kuendelea kuwasemea wananchi juu ya kero zinazowasumbua hadi kuzifikisha *ofisini kwa mkuu wa mkoa.*
Kwa upande wao *wakazi wa Kata ya Liwiti* wamefurahia kuona *migogoro yao ya muda mrefu imetatuliwa kwa mpigo* ambapo wamempongeza *RC Makonda* kwa usimamizi mzuri wa *sheria* huku wakimpongeza *Rais Dkt. John Magufuli* kwa kuwateulia *Mkuu wa Mkoa anaewafuata na kuwasikiliza wananchi wake.*
No comments:
Post a Comment