Advertisements

Saturday, July 14, 2018

SAFARI YA MWISHO YA MPENDWA WETU MZEE JAMES HANDO

Hii ndiyo safari ya mwisho ya mpendwa wetu mzee James Basil Hando iliyofanyika siku ya Jumamosi July 14, 2018 Burlington, North Carolina katika makaburi la North Lawn na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki akiwemo kaka wa marehemu Mzee Polysect Basil Hando aliyekuja toka Tanzania kumzika mdogo wake. Picha na Vijimambo Blog, NC.
Familia ikifuatilia mazishi ya mpendwa wao mzee James Hando.
Familia, ndugu, jamaa na marafiki wakimsikiliza padri Paul Lininger (hayupo pichani) wakati akiongoza ibada ya mazishi ya mpendwa wetu mzee James Hando katika safari yake ya mwisho kwenye makaburi ya North Lawn yaliyopo Burlington, North Carolina siku ya jumamosi July 14, 2018.
Safari ya mwisho ya mpendwa wetu mzee James Hando.
Mtoto wa marehemu Scolla Hando Tayn akiweka mchanga kwenye kwenye kaburi la mpendwa baba yake
Mtoto na wajukuu wakiweka maua.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Juu na chini ni picha kanisani baada ya ibada ya kumwombea mpendwa wetu mzee James Hando.
Picha juu na chini ni mazishi, utupiaji mchanga na maua ya mpendwa mzee wetu James Hando katika makaburi ya North Lawn yaliyopo Burlington, North Carolina.
 Picha Juu na chini ni nyumbani kwa wafiwa baada ya kutoka kumpumzisha mpendwa James Hando

1 comment:

Osman Kazi said...

Hatujui kesho yetu, tenda wema ili uishi vizuri....
RIP Mz Hando