Advertisements

Monday, July 23, 2018

SPRITE BBALL KINGS YAFIKIA PATAMU, TIMU NNE ZATINGA NUSU FAINALI

 Nahodha wa Timu ya Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph akijaribu kuwatoka wachezaji wa St Joseph wakati wa mechi ya robo fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings uliomalizika kwa Mchenga kuibuka na ushindi wa Vikapu 84 kwa 47 vya St Joseph.

 Vuta nikuvute wakati wa mechi ya robo fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings uliomalizika kwa Mchenga kuibuka na ushindi wa Vikapu 84 kwa 47 vya St Joseph.
Mashabiki waliojitokeza kuangalia michuano ya Sprite BBall Kings katika Uwanja wa Ndani wa Taifa.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) Phares Magessa (kulia) akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa TBF Mike Mwita wakishuhudia robo fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
ROBO fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings imefanyika mwishoni mwa wiki hii na timu nne kufanikiwa kuvuka kwenda hatua inayofuata ya nusu fainali.

Mechi hizo zilizochezwa ndani wa Uwanja wa Ndani wa Taifa zilikuwa za ushindani mkubwa sana huku Bingwa mtetezi Mchenga BBall Stars akifanikiwa kushinda na kusonga hatua inayofuata.

Katoka mchezo wa kwanza uliokwakutanisha Water Institute dhidi ya Flying Dribblers uliweza kumalizika kwa Flyinh Dribllers kuibuka na  ushindi wa vikapu 100 dhidi ya 64

Mchezo wa pili uliwakutanisha Team Kiza akichuana na DMI, na katika mchezo huo DMI walikubali kichapo cha vikapu 82 kwa 47 vya DIM.

Mchenga Bball Stars alichuana na St Joseph katika mchezo wa tatu, mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa na mpaka filimbi ya mwisho inapulizwa Mchenga akafanikiwa kuvuka kwa vikapu 84 dhidi ya vikapu 67 vya St Joseph.

Mechi ya mwisho ilikua ni Temeke Heroes dhidi ya Portland iliyohitimisha idadi ya timu nne za kuingia nusu fainali, na Portland wakihitimisha mechi hiyo kwa kuibuka mshindi kwa vikapu 83 dhidi ya vikapu 70 vya Temeke Heroes.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) Phares Magessa aliweza kushuhudia michuano hiyo akiwa sambamba na Katibu Mkuu TBF Mike Mwita na kuonyesha kufurahishwa na namna mpira wa kikapu ukirejesha heshima yake.

Baada ya matokeo hayo, Droo ya upangaji wa timu itafanyika kesho (jumatatu) ikishuhudiwa na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) na timu husika na kurushwa mubashara kupitia kituo cha EATV na EA Radio.


Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yanafanyika kwa mara ya pili yakiandakiwa na kinywaji cha Sprite na mshindi wa kwanza akijiondokea na kitita cha Shillingi Milioni 10, mshindi wa pili Milioni tatu na mchezaji bora wa michuano (MVP) akibeba Milioni 2.

No comments: