ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 28, 2018

Viongozi wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO Waendelea na Ziara Mjini Lindi

 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Bw. Babtista Kihanza akisisitiza jambo kwa ujumbe wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Manispaa hiyo mapema wiki hii ikilenga kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma katika kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
 Mwakilishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza umuhimu wa kuwawezesha Maafisa Habari kwa kuwapatia vitendea kazi ili waweze kutekeleza majukumu ya kutangaza miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Lindi hali itakayochochea maendeleo na ustawi wa wananchi. 
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Bw. Babtista Kihanza (watatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) wakati wa ziara ya ujumbe huo mkoani Lindi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashuri ya Manispaa ya Lindi Bw. Babtista Kihanza akisisitiza jambo kwa kiongozi wa msafara wa ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Gaudensia Simwanza wakati wa ziara ya ujumbe wa chama hicho katika Manispaa hiyo ikilenga kujionea utendaji kazi wa Maafisa Habari na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha mawasiliano hasa katika kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelelezwa na Serikali.
Mmoja wa Viongozi kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) ambaye ni sehemu ya ujumbe uliofanya ziara katika Manispaa ya Lindi Bw. Ndimmyake Mwakapiso akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Bw. Babtista Kihanza mara baada ya ziara ya ujumbe huo katika manispaa hiyo. PIX6. Kiongozi wa ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) uliotembelea Halmashuri ya Manispaa ya Lindi akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashuri ya Manispaa ya Lindi Bw. Babtista Kihanza mara baada ya ziara ya ujumbe huo katika Halmashauri hiyo mapema wiki hii. (Picha zote na Idara ya Habari MAELEZO)

Frank Mvungi- MAELEZO, Lindi
Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari (MAELEZO) wameanzisha utaratibu wa kufuatilia utendaji wa maafisa habari katika ngazi zote na kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na Wananchi.

Akizungumza Mjini Lindi Kiongozi wa Ujumbe kutoka TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO Bi. Gaudensia Simwanza amesema kuwa dhamira ya ziaraa katika Halmashuri ya Manispaa hiyo na maeneo mengine hapa nchini ni kuona changamoto zinazowakabili maafisa Habari katika kutekeleza jukumu la kuisemea Serikali na kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia katika kutatua changamoto zilizopo.

“ Ziara yetu inalenga kuona namna maafisa Habari wanavyotekeleza jukumu la kuisemea Serikali katika Manispaa ya Lindi hasa kutangaza miradi inayotekelezwa na Serikali kwa manufaa ya wananchi” Alisisitiza Simwanza Akifafanua Bi. Simwanza amesema kuwa Halmashuri zinalo jukumu la kuwawezesha maafisa hao ili waweze kutekeleza jukumu la kuisemnea Serikali katika maeneo yao hasa kutoa taarifa za miradi inayotekelezwa akitolea mfano wa ujenzi wa barabara za Lami katika Manispaa hiyo ambao umefanyika kwa kiwango kikubwa na kubadili taswira ya mji huo na kuwa ya kuvutia.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashuri ya Manispaa ya Lindi Bw. Babtista Kihanza amesema kuwa Ofisi yake iko tayari kuweka mazingira wezeshi kulingana na upatikanaji wa rasilimali ili kuwezesha mawasiliano kati ya wananchi na Serikali kuimarika hasa katika kutangaza miradi ya maendeleo.

“ Sisi tuko tayari kumuwezesha afisa habari wetu kadiri rasilimali zitakavyoruhusu ili aweze kufanikisha jukumu la kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.” Alisisitiza Babtista

Kwa upande wake mwakilishi wa Idara ya Habari MALEZO Bw. Casmir Ndambalilo amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wanapata taarifa za miradi ya maendeleo kwa wakati muafaka ili waweze kutumia fursa za miradi hiyo kujiletea maendeleo.

Aliongeza kuwa ni vyema maafisa habari katika Mikoa na Halmashauri wakatumia mbinu za kisasa katika kuwasiliana na wananchi katika maeneo yao kwa kutoa taarifa za miradi yote inayoteklezwa na ile inayotarajiwa kutekelezwa.

No comments: