Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wanakijiji wa Migato na kuwahimiza kujitola katika kufanya shughli za kujiletea maendeleo wakati mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu.
Wananchi wa kijiji cha magito wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile( hayupo pichani) mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na mtoto mkaziwa Kijiji cha Migato mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Na WAMJW Simiyu
Wananchi wa Kijiji cha Itindilo Wilaya ya Itimilo, Nangale na Migato vilivyopo Wilaya ya Itimila mkoani Simiyu wameungana kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuleta maendeleo kwa kuchangia nguvu kazi zenye thamani ya Shilling Millioni 24 kujenga Zahanati na kituo cha Afya vijiji hapo.
Hayo yamebainika wakati Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akikagua huduma za Afya na Maendeleo ya Jamii katika mkoa wa Simiyu.
Taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ikindilo imesema kuwa mradi huo unaogharimu jumla ya shilling 541,000,000 Shillingi 250,000,000 kutoka Serikalini, Shillingi Millioni 275,000,000 kutoka wadau wa Maendeleo UNFPA na Shillingi Millioni 16 kutokana na nguvu za wananchi.
Pia mradi ujenzi wa wodi ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya Kijiji cha Nangale unaogharimu jumla ya shilling 36,321,000 Shillingi 30,000,000 kutoka Serikalini kwa kushirikiana na UNFPA, na Shillingi Millioni 6,321,000 kutokana na nguvu za wananchi.
Kwa upande wa mradi wa wodi ya mama na Mtoto katika Zahanati ya Kijiji cha Migato unaogharimu jumla ya shilling 32, 4000, 000 Shillingi 25,800,000 kutoka Serikalini, Shillingi Millioni 30,000,000 kutoka wadau wa Maendeleo UNFPA na Shillingi Millioni 2 kutokana na nguvu za wananchi.
Aidha Naibu Waziri Dkt. Ndugulile amewapongeza wananchi wa vijiji cha Ikindilo, Nangale na Migito kwa kujitoa katika shughuli za Maendeleo kwa kuchangia nguvu zao.
"Nguvu kazi yenu wana Itindilo ndio nguvu ya Maendeleo katika maeneo yenu" alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Itimilo Mhe. Benson Kilangi amesema kuwa uongozi wa Wilaya uliamua kuhamasisha wananchi kuchangia nguvu zao katika kuunda kamati za ujenzi wa ujenzi wa Zahanati na Kituo cha Afya katika Vijiji vya Wilaya hiyo.
Mhe. Kilangi ameongeza kuwa wananchi walipata hamasa kubwa kutoka kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata Wilaya na Mkoa na kuwezesha kupata nguvu kazi katika mradi hiyo.
No comments:
Post a Comment