Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao hii leo Jijini Dodoma.
Waziri Mhagama ametengua Bodi ya Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Utenguzi huo umeanza hii leo tarehe 24 Julai, 2018, baada ya hatua mbalimbali za Serikali ya Awamu ya Tano kuendelea kuimarisha utendaji kazi wa Taasisi na Mashirika yake.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (MB) alipokutana na waandishi wa habari hii leo Mjini Dodoma Julai 24, 2018.
Waziri Mhagama alieleza kuwa, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo kama Waziri wenye dhamana kwenye masuala ya hifadhi ya jamii ninatangaza rasmi kuivunja Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii pamoja na uteuzi wa Wajumbe wote wa bodi hiyo.
“Lengo kuu la madiliko haya ni kuhakikisha kuwa shirika hilo linaimarishwa zaidi sambamba na kusimamia mwenendo wa kila siku wa shirika ikiwemo zile kazi za msingi kuongeza wanachama, kukusanya michango, kulipa mafao kwa wakati na kusimamia vitega uchumi kwa uzalendo na weledi” alisisitiza Mhagama
Aidha, Waziri Mhagama alitoa taarifa rasmi kuhusu mfumo utakao tumika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya Mashujaa ambayo hufanyika tarehe 25 Julai kila mwaka. Katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, fedha zilizopangwa kufanyia maandalizi ya sherehe hizo Kitaifa ambazo ilikuwa zifanyike kwenye Jiji la Dodoma zitatumika kuboresha miundombinu ya barabara katika Jiji la Dodoma.
“Mwaka huu 2018 hakutakuwa na maadhimisho ya pamoja ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa, baadala yake kila Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji watafanya maadhimisho ya siku hiyo kwa kufanya usafi katika maeneo waliyozikwa Mashujaa wetu na maeneo yoyote ambayo yanakumbukumbu za Mashujaa wetu nchini” Alisema Mhagama.
No comments:
Post a Comment