ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 22, 2018

Waziri Mkuu wa Korea atembelea NIDA na Hospitali ya Mnazi Mmoja

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola (Mb.) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Mhe. Lee Nak-Yon mara baada ya kuwasili kwenye kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kilichopo Kibaha. Kituo hicho kilijengwa kwa Mkopo wa masharti nafuu kutoka Korea kupitia Banki ya Exim. 
Mhe. Nak-Yon akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye kituo hicho. 
Mhe. Nak-Yon (katikati) akisiliza maelezo ya namna kituo cha kutunzia kumbukumbu cha mamlaka ya vitambulisho vya taifa kinavyotekeleza majukumu yake. wengine katika picha wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Augustine Mahiga (Mb.), Mhe. Lugola Balozi wa Korea nchini Mhe.Song Geum-young. 
Maafisa wa vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanaendelea kutolewa kwa mgeni rasmi. 
Juu na chini ni seemu ya ujumbe wa mhe. Nak-Yon pamoja na ujumbe kutoka Tanzania wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yanatolewa. 
Mhe. Nak-Yon akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara yake kwenye kituo hicho cha kuhifadhia kumbukumbu cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). 

*******Hospitali ya Mnazi Mmoja*******
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo (Mb.) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Mhe. Lee Nak-Yon mara baada ya kuwasili kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja. Katika hospitali hiyo, Mhe. Waziri Mkuu alipata fursa za kutembelea wagonjwa na kujionea utendaji kazi kwenye hospitali hiyo. Aidha, alipewa nafasi ya kumchagulia jina mtoto aliyezaliwa siku chache zilizopita hospiyalini hapo. Mhe. Nak-Yon pia alikabidhi msaada wa Magari mawili ya kubebea wagonjwa kwenye hospitali hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam tarehe 22.07.2018. 
Mhe. Jafo akimtambilisha kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema mara baada ya kuwasili hospitali ya Mnazi Mmoja. 
Mhe. Nak-Yon akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Madaktari wa Mmnazi mmoja kuhusu matumizi ya kifaa cha maabara. 
Mhe. Nak-Yon akisalimiana na wagonjwa waliokuwepo hospitalini hapo 
Mhe. Nak-Yon akimkabidhi zawadi mmoja wa wamama aliyejifungua Mtoto wa kike ambaye mtoto wake alipewa jina Laura na Mwaziri Mkuu huyo. 
Mhe. Nak-Yon akikabidhi msaada wa magari mawili ya kubebea wagonjwa kwa Mhe. Jafo mara baada ya kumaliza kuitembelea Hospitali hiyo. 
Mhe. Nak-Yon akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria tukio la kukabidhiwa kwa magari hayo. 

No comments: