ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 11, 2018

DKT TIZEBA AWAHAKIKISHIA WASINDIKAJI WA PAMBA KUJIAMINI SOKO LIPO LA KUTOSHA

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.(Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.
Wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na waendeshaji wa soko la bidhaa nchini Tanzania Merchantile Exchange (TMX) wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.

Na Mathias Canal, WK-Mwanza

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amewahakikishia wanunuzi na wasindikaji wa zao la Pamba kuendelea kununua na kusindika pamba kwa wingi kutoka kwa wakulima kwani soko la zao hilo kwa sasa limeimarika kwa kiasi kikubwa.

Waziri Tizeba ametoa kauli hiyo juzi tarehe 9 Agosti 2018 wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwanza Hoteli Jijini Mwanza.

Katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwapatia uelewa wanunuzi wa zao la Pamba Mhe Tizeba alisema kuwa kuna njia mbadala zaidi ya waliyonayo sasa ya kuuza Pamba yao katika soko la bidhaa ambapo bidhaa hushindanishwa kutokana na ubora wake kwa wanunuzi walio wengi Duniani.

Alisema kuingia kwenye ushindani wa soko ni miongoni mwa njia muhimu na madhubuti kwao kwani itaongeza thamani ya zao hilo hivyo kuwa na kipato kikubwa kitakachoongeza tija na mafanikio ya kipato.

Tanzania Merchantile Exchange (TMX) inawakutanisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa kwa pamoja na kwa wingi ili washindane katika bei jambo ambalo litawafanya wauzaji kuuza bidhaa zao kwa kiasi kizuri cha fedha na kupelekea kupata bei nzuri.

Katika mkutano huo Mhe Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba aliwataka wanunuzi hao kujifunza namna ambavyo soko la bidhaa Tanzania Merchantile Exchange (TMX) linafanya kazi Kwa kupeleka kiasi cha Pamba kilichozidi kutokana na mkataba walioingia na wanunuzi wao Nje ya nchi ili kujionea manufaa yaliyopo.

Hata hivyo Mhe Tizeba aliwataka wanunuzi hao kuendelea kununua Pamba kwa wakulima bila wasiwasi wowote, kwani soko la bidhaa litaweza kutumika kwa manufaa makubwa kuuza Pamba yao na kumhakikishia mkulima soko.

Alisema kuwa Katika ngazi ya uzalishaji ni muhimu sana ubora wa pamba ukaimarishwa ili soko la bidhaa liweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Aidha, Mhe Tizeba ameilekeza TMX kukutana na kampuni zinazonunua pamba mmoja mmoja ili kubaini kampuni ambazo zitaweza kuanza msimu huu kutumia soko la bidhaa

No comments: