Advertisements

Saturday, August 4, 2018

MCHAKATO WA KUANZISHA MAMALAKA YA HIFADHI ZA FUKWE WAIVA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano ya Mto Ruvuma wilaya ya Mtwara vijiji mkoani Mtwara katika ziara yake ya kikazi mkoani humo kwa ajili ya kubainisha vivutio vya utalii.

Kaimu Mhifadhi Mfawidhi Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano ya Mto Ruvuma, Jennifer Simbu akisoma taarifa kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga alipotembelea eneo hilo ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani humo kwa ajili ya kubainisha vivutio vya utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  akizungumza na watumishi wa Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano ya Mto Ruvuma alipotembelea eneo hilo  ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani huo kwa ajili ya kubainisha vivutio vya utalii
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa pamoja na watumishi  wakiangalia mandhari ya Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano ya Mto Ruvuma wakati alipotembelea eneo hilo  ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani huo kwa ajili ya kubainisha vivutio vya utalii
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akipewa maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mfawidhi wa Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano ya Mto Ruvuma , Jennifer Simbu wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea eneo hilo ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani huo kwa ajili ya kubainisha vivutio vya utalii

Baadhi ya Mandhari ya Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano ya Mto Ruvuma ambacho ni kivutio kikubwa cha Utalii kwa mikoa ya kusini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano ya Mto Ruvuma Wilaya ya Mtwara vijijini wakati alipotembelea eneo hilo ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara kwa ajili ya kubainisha vivutio vya utalii 

( PICHA ZOTE NA LUSUN GU HELELA-MNRT)

Wizara ya Maliasili na Utalii imesema ipo mbioni kuanzisha Mamlaka ya Hifadhi za Fukwe nchini ili ziweze kusimamiwa ipasavyo kwa kujenga miundombinu bora itakayowavutia watalii wengi na hatimaye kuongeza pato la taifa.

Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo lililotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa alipokuwa anawasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amebainisha hayo wakati alipotembelea Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano wa Mto Ruvuma katika wilaya ya Mtwara vijijini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara ya kubainisha vivutio vya Utalii vilivyopo mikoa ya Kusini.

Amesema Tanzania imejaliwa kuwa na fukwe nzuri lakini fukwe hizo zimekuwa zikitumika visivyo baadala ya kutumika kama chanzo cha mapato kupitia watalii.

Amefafanu kuwa fukwe zilizo nyingi zipo tu na zimekuwa hazina uwekezaji wa namna yeyote ile wakati ni rasilimali muhimu sana katika kuongeza pato la taifa kwa vile watalii walio wengi kwa sasa wameanza kuugeukia utalii fukwe baadala ya wanyamapori.

Akizungumzia hatua za awali ambazo Wizara inazifanya kwa sasa, Naibu Waziri huyo amesema wameshaanza mazungumzo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambayo ndio Wizara inayozisimamia fukwe hizo kwa sasa.

Kwa upande wake, Kaimu Mhifadhi Mfawidhi Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano ya Mto Ruvuma, Jennifer Simbu amesema mchakato wa kuunda Mamlaka hiyo uharakishwe ili Hifadhi hizo ziweze kuongeza pato la taifa kwa vile zitakuwa na uwezo wa kujitangaza

Aidha, Mhifadhi huyo Jennifer Simbu amesema mwaka 2010 kuna baadhi ya Wawekezaji walijitokeza wakitaka kuwekeza lakini hadi hivi sasa hakuna hata Mwekezaji hata mmoja kati ya watano waliopewa maeneo hakuna aliyeyaendeleza.

No comments: