ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 28, 2018

MTOTO DARASA LA 5 ADAIWA KUUAWA KWA KIPIGO CHA MWALIMU

MWANAFUNZI wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kibeta, Sperius Eradius (13) amefariki dunia akidaiwa kupigwa na mwalimu wake kwa kutuhumiwa kuiba pochi ya mwalimu wilayani Bukoba, mkoani Kagera jana, Jumatatu, Agosti 27, 2018.

Baadhi ya wanafunzi walioshuhudia tukio hilo lililotokea jana wamesema mwanafunzi huyo alikwenda kumpokea mizigo mwalimu wake aliyefika shuleni hapo kwa usafiri wa bodaboda.

Alipoingia ofisini Mwalimu huyo alianza kulalamika kutoiona pochi yake ndipo Sperius alipoitwa na kuhojiwa lakini akakana kuichukua hali iliyosababisha kuanza kupigwa akitakiwa kuirejesha.

Aidha, waliongeza kuwa baadaye walitakiwa kuitafuta pochi hiyo hadi chooni, lakini hawakuiona huku mwanafunzi huyo akiendelea kuadhibiwa. Hata hivyo, dereva bodaboda alifika shuleni hapo akimtafuta mwalimu aliyepoteza pochi na kumkabidhi pochi aliyokuwa ameisahau kwenye pikipiki yake.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoani humo, Dkt. John Mwombeki, alikiri kupokea mwili wa mtoto huyo majira ya saa mbili asubuhi ukionekana kuwa na majeraha.

CHANZO: Jamii Forum

No comments: