Advertisements

Monday, August 6, 2018

TFF, KCB WASAINI MKATABA MPYA

Picha
BENKI ya KCB imeendelea kuwa sehemu ya wadhamini wa Ligi Kuu Bara baada ya jana kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuidhamini ligi hiyo.

Akizungumza wakati wa kutia saini Dar es Salaam jana, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB, Fatma Chiro alisema mkataba huo wa shilingi milioni 420 una lengo la kuimarisha Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya ule wa awali kwisha.

Akifafanua zaidi kuhusu udhamini huo, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Cosmas Kimario alisema wameamua kuongeza mkataba mpya ili kuzisaidia klabu katika kukuza uchumi.

Aidha, alisema benki yake inaangalia uwezekano wa kudhamini pia ligi daraja la kwanza, ligi ya wanawake na ligi ya Zanzibar.

TFF imeendesha ligi ya wanawake kwa msimu wa pili sasa lakini imekuwa ikisuasua kutokana na kukosa udhamini.

Akizungumza baada ya kutia saini, rais wa TFF, Wallace Karia alisema:

“Tumekubaliana KCB waongeze mkataba baada ya ule wa awali kumalizika, benki hii ni mdhamini mzuri ambaye uongozi wa TFF umeridhia kufanya nao kazi tena,’’ alisema.

-HABARI LEO

No comments: