Advertisements

Thursday, August 9, 2018

WANANCHI MKOA WA MANYARA WANUFAIKA NA MRADI WA MIVARF

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi na Watendaji alipowasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwa ziara ya kukagua mradi wa MIVARF Mkoani Manyara, Agosti 7, 2018. (Kushoto) Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Manyara Bw. Simon Lulu, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw. Alexander Mnyeti na Mbunge wa Mbulu Mhe. Flatei Massay.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi huo Mkoani Manyara. (Kushoto) Afisa Kiungo Mradi wa MIVARF Manyara, Bi. Lulu Kaaya, Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ester Mahawe, Katibu Tawala Msaidizi Eng. Mary Mbowe na Bw. Kennedy Kaganda (AAS)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi, watendaji na baadhi ya wateja wa CRDB, alipofanya ziara Mkoani Manyara na kufanikiwa kukagua benki ya CRDB iliyoanza kutoa huduma za kifedha, kata ya Magugu.
Muonekano wa daraja la Masware ambalo kwa sasa linaunganisha vijiji vya Masware, Gochameda, Magugu na Kiru.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara

NA MWANDISHI WETU:

Serikali imeendelea kuwainua wananchi kiuchumi nchini kupitia mradi wa Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) unaolenga hususan maeneo ya vijijini.

Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) alisema kuwa Serikali kupitia mradi huo imefanya kazi kubwa sana kwa kuboresha miundombinu ya masoko na huduma za kifedha kwa wakulima na wananchi maskini. Mradi huu umekuwa na faida nyingi sana ikiwemo kuongeza thamani ya mazao kutokana na ujenzi wa magala ya kuifadhia mazao, miundombinu ya barabara ambayo imewezesha usafirishaji wa mazao kwenda kwenye soko kiurahisi na hivyo thamani ya mazao hayo itaongezeka na huduma za kifedha zimeweza kuwa karibu na wananchi wanauwezo wa kutunza fedha zao benki na vilevile kupata mikopo.

“Mradi huu ukawe wa mfano na wananchi wahakikishe unakuwa endelevu kwa kutunza vizuri maghala, masoko, mashine na miundombinu, kwa kufanya hivyo hii miradi itaendelea kudumu na itaendelea kutoa huduma iliyokusudiwa na uchumi wa mwananchi kukua” alisisitiza Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana wa kijiji cha Magugu kuchangamkia fursa zilizopo nchini kwa kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyoweza kuwa kwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mbunge la Babati Vijijini, Mhe. Vrajil Jituson amesema kuwa wakazi wa vijiji vya Maswale, Magugu n.k wamenufaika na mradi huo kwa kutengenezewa barabara, madaraja na magala ya mazao ambayo yamewasaidia wananchi kukua kiuchumi na upatikanaji wa huduma nyingine za kijamii.

“Mradi wa MIVARF umeinua hali ya uchumi vijijini ambapo kijiji cha Matufa, Masware, Kichameda na Magugu vimenufaika. Kwani kwa sasa wakazi wa vijiji hivyo wameweza kujiajiri kwenye kilimo cha mpunga kutokana na uwepo wa miundombinu ya uhakika” alisema Kaaya

Aidha, Afisa Kiungo Mradi wa MIVARF Manyara, Bi. Lulu Kaaya ameeleza kuwa ujenzi wa miundombinu na ghala kumefanya wakazi wa maeneo haya kuanzisha vikundi mbalimbali vya kilimo ikiwemo kikundi cha AMCOS ambao wamekuwa wakilima mpunga kwa sehemu kubwa kutokana na thamani ya mazao imeongezeka na tunauhakika wa sehemu ya kuyatunza.

No comments: