Akisomewa hati ya mashtaka jana Septemba 25, 2018 mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi, Erick Marley, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Ramsoney Salehe amedai tangu 2015 mshtakiwa alikuwa akiishi kinyumba na mwanaye mwenye umri wa miaka 17.
Imedaiwa kuwa huyo alipata ujauzito na mimba ikaharibika na mwaka 2016 akapata mimba ya pili na kujifungua mtoto wa kike ambaye alifariki mwaka huo huo na sasa amejifungua mtoto ana wiki mbili na ana ubini wa baba.
Amesema wamebaini jambo hilo kwa kuwa katika kadi hiyo, jina la baba linasomeka, Jacob Shabani ambapo Salehe ameiileza mahakama kuwa upelelezi umekamilika na shauri hilo kinaweza kusikilizwa na kuna mashahidi wanne na kielelezo cha kadi ya kliniki.
Hakimu Marley ameahirisha kesi hiyo ya jinai namba 74 ya mwaka 2018 hadi Oktoba 2, 2018 na mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kwa kukosa mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh1milioni. GPL
No comments:
Post a Comment