ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 10, 2018

HABARI KATIKA PICHA

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania-GST) iliyopo chini ya wizara ya Madini ikishirikiana na KIGAM & Geogeny Consultancy Group Inc kutoka Jamuhuri ya Korea inafanya upimaji wa kina wa kijiofizikia mkoa wa Ruvuma katika wilaya ya Songea na Tunduru (takribani kilomita 75 mashariki ya Songea) ili kukusanya takwimu na taarifa za kijiofizikia ambazo zitabaini uwepo kwa madini na mipasuko ya miamba chini ya ardhi katika maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya mradi. Upimaji huo unafanyika chini ya Mradi unaotekelezwa na African Minerals Geosciences Initiative (AMGI) Pilot Project.
Pichani ni watalaam kutoka GST na KIGAM wakijadiliana kitalaam juu ya uchukuaji takwimu na taarifa za kiutafiti zinachukuliwa na Ndege.

No comments: