Advertisements

Tuesday, September 25, 2018

TABORA WAWAOMBEA WANANCHI WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA MV NYERERE

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za wakazi wa Tabora wakati wa maombi ya kuombea marehemu wa ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.
 Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya akitoa salamu za wakazi wa Manisapaa ya Tabora wakati wa maombi ya kuombea marehemu wa ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.
 Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri  akitoa salamu za wakazi wa wilaya yake wakati wa maombi ya kuombea marehemu wa ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.
 Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo  akitoa salamu za wakazi wa Igunga wakati wa maombi ya kuombea marehemu wa ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.
 Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Janeth Kayanda  akitoa salamu za CCM wakati wa maombi ya kuombea marehemu wa ajali ya MV Nyerere  wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.
 Wanachuo wa Chuo cha Ualimu Tabora wakiimba wimbo maalumu wa kuwakumbuka Watanzania waliopteza maisha kwenye ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.
 Shekh wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi akiongoza dua ya kuwaombea wananchi walipoteza maisha kwenye ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao..
 Askofu wa Anglikana Tabora,Elias Chakupewa akiongoza maombi ya kuwaombea marehemu waliopoteza maisha katika ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao..

Viongozi mbalimbali mkoani Tabora wakiwa katika maombi maalumu ya kuwaombea wananchi waliopoteza maisha katika ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.

NA TIGANYA VINCENT
WAKAZI wa Mkoa wa Tabora wamekutana kwa ajili ya kuwaombea wananchi waliopoteza maisha yao  baada ya kuzama meli ya MV Nyerere tarehe 20 Mwezi huu katika Kisiwa cha Ukara mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa maombi hayo jana jioni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema Taifa limepoteza nguvu kazi kubwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi na kuwaacha wananchi wakiwa katika simanzi kubwa.

Alisema miongoni mwa waliofariki kuna watoto huku watu wakipoteza wenza wao na hivyo kubaki wagane na wajane na kuzifanya baadhi ya familia kuanza maisha ambayo hawakuyatarajia.

Mwanri alisema ni kipindi kigumu lakini ni vema wakamshuku Mungu na waendelee kumutegea  yeye katika kipindi hiki kwaku ndiye msaada wao wa kwanza.

Naye Mkuu wa wilaya ya Igunga,John Mwaipopo,aliwapongeza wananchi kwa kuendeleza mshikamano na umoja kwa vile baadhi ya watu walitoa maneno ambayo yangeweza kuyumbisha mshikamano na umoja uliopo.

Kwa pande wa  Askofu wa Anglikana Tabora,Elias Chakupewa alisema kuwa Biblia inasema siku za kuishi mwanadamu ni miaka sabini hadi themanini na zaidi ya hapo ni tabu na mateso makubwa na kusema kuwa baadhi ya waliofariki walipaswa kufikia miaka sabini lakini hawakufika umri huo na hivyo kuacha majonzi mengi.

Aliwataka wananchi ambao bado wako hai kutumia somo hilo la ajali hiyo kujiandaa kihoro kwani hajui watakufaje na lini.

Maombi ya Mkoa wa Tabora yaliwashirikisha viongozi wa Dini zote, wanafunzi, wananchi na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.

No comments: