Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua moja ya boksi kalvati kati ya 32 yanayojengwa katika barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndibalinze (mwenye koti la kijivu), mara bada ya kukagua moja boksi kalvati katika ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua kokoto zitakazotumika katika ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akisisitiza jambo kwa Mkandarasi kutoka kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO), Mhandisi Li, mara baada ya kukagua kokoto zitakazotumika katika ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
Kaimu Mhandisi Mkazi, Mhandisi Regnard Kaganga, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, kuhusu hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami wakati Waziri huyo alipokuwa akikagua mradi huo, mkoani Tabora.
Muonekano wa kazi zikiendelea za ujenzi wa tabaka la kifusi kiwango cha G7 katika barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora. Ujenzi wa sehemu ya barabara hiyo itaunganisha mji wa Manyoni na wa Tabora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amemtaka mkandarasi wa kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO), anayejenga barabara ya Nyahua –Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kukamilisha barabara hiyo ifikapo mwezi Desemba 2020 badala ya Machi 2021.
Amezungumza hayo mkoani Tabora, wakati akikagua hatua za maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 117.9 na kuridhishwa na ubora wa kazi zilizoanza kutekelezwa.
Amemtaka mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi ambao umefikia asilimia 12 ikiwa ni nyuma ya mpango kazi kwa asilimia 4.
Waziri Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (KFAED) na kukamilika kwake kutafungua mkoa wa Tabora na mikoa ya Katavi na Kigoma katika kukuza uchumi wa wananchi.
Waziri Mhandisi Kamwelwe, amefafanua kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu katika kukuza biashara na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani.
Aidha, Waziri Kamwele ameonesha kusikitishwa kwa vitendo vya baadhi ya wananchi kuhujumu miundombinu ya barabara ikiwemo alama za barabarani hasa katika mkoa huo na kuomba kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kusaidia Serikali katika kudhibiti.
"Kuna watu huku Tabora waliokamatwa na vyuma vya alama za barabarani majumbani mwao wakitwangia mahindi, hili suala halikubaliki na yeyote atakayepatikana sheria kali zitachukuliwa dhidi yake na Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi zaidi ili kudhibiti suala hili", amefafanua Waziri Kamwelwe.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze, amemueleza Waziri huyo kuwa ujenzi wa barabara hiyo utahusisha ujenzi wa madaraja makubwa mawili, makalvati yenye pembe nne 32 na makalvati ya mduara 60.
Akizungumzia changamoto za mradi, Mhandisi Ndabalinze amemueleza Waziri kuwa sehemu ya mwanzo ya mradi yenye urefu wa KM 1.7 ipo kwenye bonde ambalo kwa kipindi cha mvua za mwaka huu lilifurika kwa zaidi ya siku saba na kusababisha kufunga barabara hiyo ambapo eneo hilo sasa linajengewa makalvati ya pembe nne yasiyopungua saba na kujazwa mawe kwa zaidi ya mita moja juu ya tabaka la mchanga.
Waziri Mhandisi Kamwelwe yupo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Tabora ikiwa ni lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea mkoani humo
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment