Mnofu ukiendelea kuchomeka kwenye family picnic nacookout iliyoandaliwa naShield Our Watoto (SOW) kwa ajili yakuchangisha fedhana kutoaelimukwa watoto na wazazi jinsi ya kuwakinga watoto katika unyanyasaji wa kijinsia ambao katika Dunia ya leo watoto wengi hukumbana navyo huku wahusika wakuu wakiwa watu wa karibu na familia zao. Picha na Vijimambo Blog.
Mshereheshaji na mmoja ya waratibu wa SOW, Peter Kirigiti akiendeshafamilypicnic na cookout iliyofanyika siku ya Jumamosi Cot 6, 2018 Columbus, Ohio.
Baadhi ya vitu vikiuzwa kwa ajili ya kuchangia SOW iendelee kutimiza ndoto yake ya kusaidia nakuelimisha watoto wanao nyanyasika kijinsia.
Bhoke Mukami Kirigiti akiwashukuru wote waliofika na kutoa elimu kwa wazazi na watoto waliofika kwenye shughuli hiyo.
Waratibu wa SOW wakiwa katika picha ya pamoja.
Watoto wakipewa elimu ya kuweza kumjua mtu aliyedhamiria kuleta madharakwa mtoto
Baadhiya wadau wakitunukiwa vyeti vya utambuzi na shukurani kwakazi ya kujitokea walifanya katika kuhakikisha shughuli ya SOW inafana.
Baadhi ya wadau na familia zao waliohudhuria sherehe hiyo.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Waratibu wa family picnic na cookout yaShield Our Watoto wakifanya maandalizi ya kuwatunuku vyeti vya shukurani kwa utambuzi wa kazi kubwa ya kujitolea katikakuhakikisha shughuliya SOW inaenda vizuri.
Juu na chini Mkurugenzi wa Shield Our Watoto Bhoke Mukami Kirigiti akiwa kwenye zoezi la kutunuku vyeti vya utambuzi vya shukurani kwa baadhi ya wadau waliojitolea kusaidia shughulihiyo nakuhakikisha imefana.
No comments:
Post a Comment