Siku ya Ijumaa Oct 26, 2018 SHINA ilisherehekea miaka 16 tangu kuanzishwa kwake DMV. Katika sherehe hiyo iliyokua na lengo la kuchangisha fedha zitakazotumika katika kusaidia watu mbalimbali barani Afrika wenye mahitaji mbalimbali katika sekta ya afya, elimu na kutoa misaada kwa watu wasiojiweza hususani walemavu kwa lengo la kuleta unafuu katika maisha yao ya kila siku.
Katika maadhimisho hayo ya kusherehekea miaka 16, wadau na mashuhuda wengi waliongea mengi na kuipongeza SHINA kwa yote wanayofanya katika kuhakikisha hakuna familia inayohitaji itakayo achwa nyuma.
Miaka 16 sio mchezo ina mabonde na milima, Rais wa SHINA Bi. Jessica Mushala aliongea na kuwashukuru wote kwa kuja kuunga mkono juhudi za taasisi hiyo isiyokua ya kiserikali na kuelezea mipango ya baadae ikiwemo kwenda Nigeria kwa lengo la kufikisha huduma za afya, elimu na mambo mengine kwa wahitaji wasiokua na uwezo.
Msemaji mkuu Bwn. Jamal Walkings alisema kila mtu anathamani hapa Duniani, kwa kile unachoweza kukifanya kiwe kikubwa au kidogo ni mchango unaoonyesha uthamani wako.
Bwn. Jamal Walkings ambaye ni kijana mdogo mwenye uwezo wa kuongea mambo makubwa anayesoma katika chuo kikuu cha Maryland Eastern Shore anayeendesha kipindi cha mazungumzo ya kila wiki katika Radio ya UMES Hawk, alimalizia kwa kuipongeza SHINA kwa kile wanachofanya kwa kutambua thamani ya watu wengine kwa kuwanyanyua na kuwafanya watambue thamani yao hapa Duniani.
Amos Mushala akielezea historia ya SHINA na jinsi ifanyavyo shughuli zake. Picha na Vijimambo Blog
Rais wa SHINA Bi. Jessica Mushala akitoa shukurani zake kwa wadau wanaoungamkono SHINA kwa kila jambo wanalofanya.
Bwn. Jamal Walkings ambaye ndiye aliyekua msemaji mkuu akiongea.
Washerehesahi kushoto ni Primrose (kushoto) na Bwn. Dulo wakiwa kazini.
Mchungaji Francis Forsang akifungua maadhimisho ya miaka 16 ya SHINA kwa maombi.
Wageni waliohudhuria maadhimisho hayo ya kusherehekea mia 16 ya SHINA wakifuatilia maombi.
Mwimbaji wa nyimbi za injili Rose Kachuchuru akiimba moja ya nyimbo zake.
Bi Pamela Nfor (mwenye kipaza sauti) akilia baada ya kuelezea jinsi gani SHINA walivyomsaidia na jinsi walivyotoa misaada Cameroon baadae alitokwa na machozi ndipo pichani Rais wa SHINA Bi. Jessica Mushala, Amos Mushala na Primorose walipomfuata na kumtuliza.
Kulia ni Bi.Lisa Polgar akielezea jinsi gani anavyifahamu SHINA na kuwashukuru kwa wanachofanya. Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
No comments:
Post a Comment