Advertisements

Thursday, October 11, 2018

UPDATES: POLISI YASEMA MO DEWJI BADO HAJAPATIKANA

Image result for mo dewji
JESHI la polisi nchini limesema juhudi za kumpata mfanyabiashara Mohammed Dewji (Mo) ambaye anasemekana ametekwa na watu alfajiri ya leo eneo la Oyster Bay jijini Dar es Salaam katika gym ya Collosseum, bado hazijazaa matunda.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa mchana huu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo ambapo Mo alikamatwa sehemu hiyo alikokuwa amekwenda kwa ajili ya mazoezi.

Mambosasa alikuwa anakanusha uvumi kwamba mfanyabiashara huyo na mwekezaji katika Klabu ya Simba ya Dar es Salaam alikuwa amepatikana eneo la Coco Beach Dar es Salaam.

“Hata hivyo kuna baadhi ya watu tunawashikilia kuhusiana na tukio hilo kwa ajili ya mahojiano lakini kwa sasa siwezi kuwataja idadi yao lakini tumejipanga vilivyo katika mikoa yetu yote mitatu. Ukaguzi unaendelea kufanyika katika vizuizi vyote vya barabarani ili kuhakikisha hakuna mhusika yeyote wa tukio hilo ambaye atapa nafasi ya kukimbia,” alisema na kuwaomba wananchi kuwa watulivu na kuendelea kushirikiana na polisi kwa karibu na kwamba taarifa rasmi za tukio hilo watazipata kutoka jeshi la polisi na siyo kwingine.

Katika hatua nyingine baada ya taarifa kwa Mo, gazeti la michezo la Championi Ijumaa lilifika makao makuu wa Klabu ya Simba, Kariakoo, ambapo hali ilikuwa shwari, bila kuwepo makundi ya wapenzi na wanachama wake kama ilivyozoeleka

No comments: