Advertisements

Thursday, October 11, 2018

DKT TIZEBA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI HATI YA MARIDHIANO UKOPESHAJI WA MATREKTA

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB), Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Ndg Marco Mtunga na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Prof Damian Gabagambi wakionyesha hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.

Na Mathias Canal-WK, Morogoro

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba leo tarehe 11 Octoba 2018 ameshuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Mikutano katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro Waziri Tizeba amesisitiza matrekta hayo kutumika ipasavyo kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo nchini jambo litakalokuwa na manufaa kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Taasisi ambazo zimeshirikiana kufanikisha utiaji saini huo ni Bodi ya Pamba ambayo ipo chini ya wizara ya kilimo, Benki ya Maendeleo ya kilimo-TADB, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Tume ya Maendeleo ya ushirika.

Dkt Tizeba alisema kuwa Vyama vya ushirika vya msingi vinapaswa kuongeza juhudi katika kilimo ili kuakisi kulipa gharama za mkopo ambao ni asilimia 20 ya mkopo wote katika kipindi cha miaka mitatu huku asilimia zingine 80 zikilipwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo-TADB.

Utiaji huo wa saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta 300 kwa vyama vya msingi vya ushirika unajili wakati ambapo hivi karibuni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwaalimkabidhi Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba jumla ya matrekta 500 ya Ursus kwa ajili ya kukopeshwa kwenye vyama vya ushirika vya msingi ili wakulima kunufaika na tija katika kilimo hususani zao la Pamba.

Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini Dkt Tizeba alisema kuwa sekta ya kilimo nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tija ndogo inayosababishwa na matumizi madogo ya pembejeo, huduma duni za ugani na matumizi ya zana duni za kilimo ambapo wakulima wengi wanatumia majembe ya mkono au kutumia maksai wakati wa kulima.

“Katika kilimo cha Pamba msimu wa mwaka 2017/2018 ushahidi unaonyesha wakulima walichelewa kuanza kuandaa mashamba kwa sababu Maksai wakati wa kiangazi wanadhoofu sana,” Alikaririwa Dkt Tizeba na kuongeza kuwa

“Mara mvua inaponyesha hawawezi kulima mpaka majani yawe mengi ndio wapate nguvu za kuanza kulima, hali hii inaondoa uwezekano wa wakulima kutumia teknolojia mpya katika kilimo kama vile kilimo hifadhi ambacho kimedhihirika kuongeza tija zaidi ya mara mbili”

Tizeba alisema mtazamo wa mpango huo ni kuunganisha nguvu za mkulima mmoja mmoja ili kuharakisha kuleta maendeleo yao ambapo utatekelezwa kwa kutumia sehemu ya fedha zinazolipwa AMCOS kama kamisheni ya kusimamia ununuzi wa pamba ambapo matarajio ni kukusanya Bilioni 6 kama uzalishaji wa pamba utafika kilo milioni 400 kwa mwaka.

Alisisitiza kuwa Bodi ya Pamba pamoja na Tume ya Maendeleo ya ushirika zinapaswa kufuatilia kwa karibu hatua zote mwenendo wa ufanyaji kazi wa matrekta hayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa punde yanapoanza kufanya kazi yawe yanafanyiwa marekebisho ya mara kwa mara.

MWISHO

No comments: