Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa akiongozwa na wataalamu wa kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd kuangalia mwamba unaotoa maji ardhini kwa kutumia camera maalumu. Picha na Vero Ignatus.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akikagua urefu wa kisima katika kijiji cha Levolosi kata ya Kimnyaki akiwa ameambatana na wahandisi toka wizara ya maji na mamlaka ya maji safi na usafishaji jijinla Arusha AUWSA. Picha na Vero Ignatus
Na Vero Ignatus, Arusha
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa amelazimika kusitisha ziara kwa masaa mawili na nusu akisubiri kisima katika kijiji cha Levolosi Kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru kinachochimbwa kitoe maji kabla ya kwenda kusaini mkataba.
Aidha Prof. Makame Mbarawa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumrudisha Wizarani mara moja Mhandisi wa Miamba Amir Msangi kwa uzembe wa kutoonekana kwenye eneo la mradi.
Waziri alitoa agizo hilo jana wakati alipotembelea Kijiji cha Levolosi, Kata ya Kimnyaki kujionea zoezi la uchimbaji wa visima vitatu na baada ya hapo alitia saini ya mkataba wa ujenzi wa mtandao mpya wa maji,mitambo ya kutibu maji safi ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA na ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA Kanda ya Kati wenye thamani ya Sh.bilioni 520.
Prof.Mbarawa alisema serikali imeamua kuleta wataalam wake toka Wizarani ili wasimamie na kujifunza Teknolojia mpya ya uchimbaji visima vikubwa kwa ajili ya kuweza kufundiaha wenzao utaalam huo hapo baadaye.
"Lakini cha kushangaza nimepata taarifa huyu Amir Msangi haonekani eneo la kazi na hivyo namwagiza mtaalam mwenzake Fatuma Mambo kumtaarifu Katibu Mkuu ili arudishwe Wizarani huyu na hapa aletwe mwingine atakayepata ujuzi huu,"alisema
Amesisitiza kuwa lengo kubwa la serikali ni kuwaleta wataalam hao ili kuhakikisha miradi ya maji inayotekelezwa inakuwa na ubora uliokusudiwa.
Alisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia wananchi kupata maji kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2020.
Aidha alisema miradi hiyo inatekelezwa na AUWSA kwa ufadhili wa serikali kupitia mkopo wa masharti nafuu toka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Arusha (AUWSA) Mhandisi Ruth Koya alisema mradi huo utakamilika Juni mwaka 2020 na wanatarajia Arusha itanufaika na mradi huo kwa kuwa ukosefu wamaji utakua historia.
"Kwa kuanza tayari wakandarasi wameanza kusambaza mabomba ya maji taka nakuweka ya kisasa na makubwa yanayoendana na mahitaji ya sasa,lengo mazingira yawe safi na wananchi wapate huduma zamaji safi bila shida,"alisema
Mhandisi Koya alisema zaidi ya wananchi 827,000 watanufaika na mradi huo ambao utazalisha maji lita milioni 200 kwa siku.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya AUWSA, Dk.Richard Masika alisema ili miradi hiyo inayotekelezwa sasa iwe mfano na endelevu wamewapatia mafunzo Timu ya Menejimenti na watumishi wengine toka kwa wataalamu wa Jumuiya ya kusimamia mikataba ya Kimataita.
"Ikukwepa gharama serikali tulimgharamia kuleta wataalam hawa toka nchi ya Switzerland"
No comments:
Post a Comment