Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, 9NSSF), jijini Dodoma Jumamosi Oktoba 27, 2018
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amezindua Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF), jijini Dodoma Jumamosi Oktoba 27, 2018.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Jenista Mhagama amesema, Bodi hiyo inayoongozwa na Balozi Ali Iddi Siwa imeteuliwa kwa kufuata matakwa ya sheria zinazoongoza sekta ya hifadhi ya jamii na sheria ya mdhibiti SSRA.
Mhe. Waziri alisema, moja ya changamoto zinazoikabili sekta ya hifadhi ya Jamii ni kuwa na wigo mdogo wa idadi ya Watanzania waliojiunga na sekta hiyo.
“Hatujafanya vizuri sana katika sekta isiyo rasmi, ni watanzania wachache sana wanahudumiwa na hifadhi ya jamii, na hao ndio wengi ukiacha wafanyakazi na kada nyingine sekta hii ndiyo ina watanzania wengi ambao hawapati huduma hii.” Alisema na kuongeza
“Kwa mujibu wa marekebisho ya sheria namba 2 ya mwaka 2018 yaliyofanyika yamekabidhi jukumu hili kwenye Mfuko wa NSSF kwa hiyo kazi hii ni yenu.” Alisisitiza.
Alisema macho ya serikali yako kwenye bodi na menejimenti ya Mfuko kuhakikisha wigo wa idadi ya wanachama kutoka sekta isiyo rasmi coverage yake inaongezeka.
“Tumejiwekea malengo ya kuongeza watanzania wengi walio katika sekta isiyo rasmi kujiunga na hifadhi ya jamii kutoka asilimia 11 na kufika asilimia 40 na tumesema lini tutafika asilimia 40 na watakaotufikisha huko ni NSSF, ni wewe Mwenyekiti amoja na bodi yako kwa kipindi ambacho mmepewa kazi ya mkuhudumia bodi hii.” Alisema.
Mhe. Waziri pia ameitaka bodi hiyo kuhakikisha kila mara inafanya tathmini na kujiridhisha kama kuna miradi itakayoanzishwa au iliyopo inasuasua bodi inapaswa kuinasua kwa kuchukua hatua na kufanya maamuzi sahihi kwa wakati ili kujenga imani kwa wanachama.” Alisema.
Wajumbe ws abode hiyo ni pamoja na Bi. Jane Nyimbo Taylor, Bw. Pelesi Jonathan, Bw.David Magese, Bw.Fred Hans Kipamila, Dkt.Elirehema J. Doriye na Bw. Ahmed A Msaki.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Dkt. Irene Isaka na viongozi wa juu wa Wizara.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi, Balozi Ali Iddi Siwa alimuhakikishia Mhe. Waziri kuwa bodi yake itafanya kazi kwa weledi na umakini mkubwa ili kufikia matarajio ya serikali ya kutoa usimamizi ulio bora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kushoto), akimkabidhi vitendea kazi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Balozi Ali Iddi Siwa, (wapili kulia), huku Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, (wakwanza kulia), Mkuerugenzi Mkuu wa SSRA, Dkt. Irene Isaka, na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Andrew Massawe wakishuhudia, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya NSSF jijini Dodoma Oktoba 27, 2018
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Andrew Massawe, akizungumza wakati w auzinduzi wa Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF), jijini Dodoma ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama,ndiye aliyezindua bodi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Balozi Ali Iddi Siwa, (aliyesimama), akitoa neon la shukrani baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama, (wapili kushoto), kuzindua bodi hiyo jijini Dodoma Jumamosi Oktoba 27, 2018.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, 9NSSF), jijini Dodoma Jumamosi Oktoba 27, 2018
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio, (aliyesimama), akitoa neon la utangulizi kabla ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe.Jenista Mhagama, (wapili kushoto), kuzindua bodi hiyo jijini Dodoma Jumamosi Oktoba 27, 2018.
Mhe. Waziri na viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja na bodi mpya ya NSSF baada ya kuizindua Oktoba 27, 2018 jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Menejimenti mpya ya NSSF. Kutoka kushoto, Mkuerugenzi wa Fedha, Gangamala Luchunga, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Gabriel Silayo, Mkurugenzi wa Masuala ya Utawala na Utumishi, Bw. Julius Mganga, Mkurugenzi wa TEHAMA, Robert Mtendamema na Mkurugenzi wa Uendeshaji Asumpta Malya.
Viongozi wa NSSF, Meneja wa sheria, Suleiman Msangi (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani, Nurdin Mruma wakibadilishana mawazo.
Meneja Mkuu wa Masoko na Uhusiano, Bi. Lulu Mengele
Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Chuma.
No comments:
Post a Comment