ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 30, 2018

WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID MOHAMMED AZUNGUMZA NA UJUMBE WA MADAKTARI WA MENO KUTOKA NCHINI UTURUKI

 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Ujumbe wa Madaktari wa Meno kutoka Nchini Uturuki huko katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
 Mratibu wa Ujumbe wa Madaktari wa Meno kutoka Nchini Uturuki Dkt. Feroz Jafferji  akitoa shukrani kwa Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed (hayupo pichani) juu ya mapokezi mazuri waliyoyapata.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Waandishi wa habari ( hawapo Pichani) kuhusu ujio wa Ujumbe wa Madaktari wa Meno kutoka Nchini Uturuki huko  Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed akiwa katika  Picha ya pamoja na Ujumbe wa Madaktari wa Meno kutoka Nchini Uturuki huko Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.


Miza Kona, Maelezo Zanzibar 
WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea ujumbe wa Madaktari 11 kutoka nchini Uturuki kwa ajili ya kutoa huduma ya meno kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba

Ujumbe huo una lengo la kutoa huduma ya meno kwa wananchi mbali mbali wa vijijini ili kuweza kupunguza tatizo la meno pamoja na kutoa taaluma ya kujiepusha na madhara ya meno huko katika hospitali ya Kivunge Wilaya yaKaskazini A Unguja

Akizungumza mara baada kuwasili ujumbe huo huko Wizara ya Afya Waziri wa wizara hiyo Hamad Rashid Mohammed amesema ujumbe wa madaktari hao una lengo la kutoa huduma ya meno pamoja na kutoa taaluma hiyo katika chuo kikuu cha SUZA ili kupata wataalamu wa meno hapa nchini

Amesema ujio huo utasaidia kusomesha madaktari wa fani hiyo ili kupata wataalamu wazalendo kwa lengo la  kuondosha upungufu wa madaktari wa  meno.

Aidha amesema madaktari hao watatoa huduma hiyo kuanzia Kivunge, Makunduchi, Tumbatu, Unguja Ukuu, Chake, Wete na Mkoani .   

No comments: