ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 12, 2018

'Amber Ruty' akosa dhamana, kuendelea kusota mahabusu

Watuhumiwa waliosambaza picha za ngono
By Tausi Ally, Mwananchi tally@ mwananchi.co.Tz

Dar es Salaam. Mcheza Video, Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Ruty' anayekabiliwa na makosa mawili ikiwamo la kufanya mapenzi kinyume na maumbile ataendelea kusota rumande baada ya kukosa dhamana.

Mbali na Amber Ruty mshtakiwa mwingine anayeendelea kusota rumande kwa kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili kila mtu na kusaini bondi ya Sh15 milioni ni Said Bakary.

Wadhamini hao, wanatakiwa wawe na vitambulisho vya Taifa na washtakiwa hao wasalimishe hati zao za kusafiria mahakamani na wasitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.

Kwa upande wa mshtakiwa mwenzao, James Delicious yeye alifanikiwa kutimiza masharti hayo ya dhamana Novemba 2, 2018 walipofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza.

Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono leo Novemba 12 katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile amedai kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Hata hivyo, baada ya Kombakono kueleza hayo, Amber Ruty amenyoosha mkono akiwa kizimbani katika ukumbi namba 2 wa Mahakama ya wazi na kuomba dhamana.

Baada ya kutoa ombi hilo, Hakimu Rwizile ameita mahakamani hapo wadhamini wake mara kadhaa na wakili wa Serikali Kombakono naye amewaita wadhamini hao lakini hakuwepo hata mmoja.

Hivyo ameiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 26, 2018 kuwaeleza washtakiwa hao iwapo wadhamini wao watafika ndani ya muda wa mahakama watadhaminiwa.

Mbali na Amber, washtakiwa wengine ni Said Bakary Mtopali na James Charles maarufu 'James Delicious'.

Katika kosa la kwanza la kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo linamkabili Amber Ruty, inadaiwa alitenda kosa hilo kati ya ama baada ya Oktoba 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary Mtopali kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia, kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary Mtopali ambaye anadaiwa kati ya ama baada ya Oktoba 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Ruty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambalo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya Oktoba 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruty na Said Abubakary Mtopali ambao wanadaiwa kati ya Oktoba 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.

No comments: