Advertisements

Monday, November 12, 2018

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI KUJADILI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA JIJINI DODOMA

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Frolens Luoga, nje ya viwanja vya Bunge, Jijini, Dodoma, baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kujadili  Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni siku chache zijazo.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. David Silinde (Mb), akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kijitabu cha Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha, wakati kamati hiyo ilipokutana na Waziri huyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi (Mb)  na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, kujadili Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, utakaowasilishwa kwa hati ya Dharura katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Geroge Simbachawene (Mb), akizungmza jambo wakati kamati yake ilipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, na wataalamu wa Sera na Uchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma, kujadili Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Andrew Chenge (Mb) na Prof. Anna Tibaijuka (Mb) wakifuatilia kwa makini mjadala wa Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Bungeni, Jijini Dodoma, siku chache zijazo.
 Baadhi ya viongozi waandamizi kutoka Idara ya Sera ya Wizara ya Fedha na Mipango, wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Idara hiyo Bw. Mgonya Benedicto (kulia) wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, ilipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb), na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, Bungeni Jijini Dodoma, kujadili muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha unaotarajiwa kuwasilishwa na Wizara ya Fedfha na Mipango, Bungeni, Jijini Dodoma, siku chache zijazo
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Albert Obama na Mbunge wa Viti Maalum Dkt. Swale Semesi wakisikiliza hoja mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedfha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa kwa Hati ya Dharura katika vikao vya Bunge vinavyoendelea Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza Jambo mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene (Mb),  wakati wa kujadili Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni siku chache zijazo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) (katikati) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, wakiandika hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kuhusu Muswada wa Sheria Ndogo za Fedha unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma, siku chache zijazo
 Mjumbe wa Kamati ta Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hussen Bashe, akichangia hoja wakati kamati hiyo ilipokutana na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kujadili Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha ya Mwaka 2018,  unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni wakti wa vikao vya Bunge vinavyoendelea Jijini Dodoma
 Mjumbe wa Kamati ta Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. David Silinde (Mb),  akichangia hoja wakati kamati hiyo ilipokutana na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kujadili Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha ya Mwaka 2018,  unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni wakti wa vikao vya Bunge vinavyoendelea Jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ya kisheria baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kujadili Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni siku chache zijazo.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments: