JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MADINI
TAASISI YA JIOLOJIA NA
UTAFITI WA MADINI TANZANIA
S.L.P 903, DODOMA
Simu: +255 26 2323020
Nukushi: +255 26 2323020
Barua pepe: madini.do@gst.go.tz
TAARIFA YA USHIRIKI WA GST KATIKA MASHINDANO YA REMOTE SENSING KUTOKA NCHI ZA KUSINI MWAAFRIKA (SADC) TAREHE 29 OCTOBA 2018 - 02 NOVEMBA 2018.
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Remote Sensing yaliyoshirikisha nchi za kusini mwa Jangwa la Afrika (SADC) chini ya udhamini wa taasisi ya Japan Oil,Gas and Metals Extration Corporation (JOGMEC) ya nchini Japani.
JOGMEC ni taasisi ambayo ipo kwenye serikali ya Japan ambapo wameweka kituo cha Remote Sensing nchini Botswana kwa ajili ya mafunzo na mashindano ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC).
Mashindano hayo kwa mwaka huu wa 2018 yalishirikisha nchi kumi na tatu ambazo ni Zimbabwe, Tanzania, Msumbiji, Angola, Zambia, Botswana, Malawi, Lesotho, Eswatini, AfrikaKusini, DR.Congo, Madagascar na Nambia.
Nchi ya Tanzania iliwakilishwa na wataalamu watatu Hafsa M. Seif , Maswi Solomini , na Abbas Mruma wote kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST). Dhumuni la mashindano hayo ni kupima uwezo na ufahamu wa jinsi ya kutumia Remote Sensing kwenye sekta ya madini hususani katika uchakataji wa data.
Wataalamu walipewa taarifa katika mfumo wa data kutoka kwa jopo la wasimamizi ambazo ni Sensor Data (ASTER, LANDSAT, SRTM-DEM na PALSAR) taarifa hizo zilichakatwa (Processed) kwa kutumia software ya ENVI, ArcGIS na QGIS , baada ya kuchakata taarifa kila nchi walipaswa kuandaa wasilisho (presentation) kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ya kupewa alama za ushindi.
Kwa upande wa Tanzania mada ya mradi ilikuwa inahusu ‘Detection of Indicator hydrothermal alteration minerals for geothermal resources around Lake Natron’.
Kwenye mashindano hayo kulitakiwa kuwa na washindi wanne tu baada ya kufanyiwa tathimini na majaji kutoka nchini Japan ambao ni Mr Susumu Nagae, Dr Kazuyo Hirose na Dr Rentaro Shimizu , jopo la majaji lilitangaza washindi wan chi ambazo ni Tanzania, Madagascar, Afrika Kusini na Namibia ,kila mshindi alipewa kombe na cheti cha ushindi (Award Winner)
Mashindano haya ufanyika kila mwaka na udhaminiwa na JOGMEC , kwa mwaka huu yalianza tarehe 29 Oktoba mpaka 2 Novemba, 2018 nchini Botswana katika mji wa Lobatse.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania
(GST)
09/11/2018
No comments:
Post a Comment