ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 4, 2018

CGP KASIKE AFUNGUA MKUTANO WA WANGANGA WAKUU WA VITUO VYA AFYA VYA MAGEREZA NCHINI LEO DESEMBA 4, 2018

Kamishna Jenerali wa Magereza  (CGP) Phaustine Kasike akisalimiana na baadhi ya wajumbe na viongozi wa Asasi ya kiraia ya JSI AIDS Free mara alipowasili leo Desemba 4, 2018  katika viwanja vya Morena Hotel jijini Dodoma kwa ajili ya ufunguzi wa kikao cha siku moja cha kutathmini ya mwenendo  wa  Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18.
 Kamishna Jenerali wa Magereza  (CGP) Phaustine Kasike akitoa hotuba katika mkutano wa waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza yote nchini kilichoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free  kwa ajili ya kutathmini ya mwenendo wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18 leo Desemba 4, 2018 Morena Hoteli jijini Dodoma.  Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Omary Salum, Mtendaji Mkuu wa AIDS Free Tanzania Dkt. Deogratias Kakiziba. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza INSP Adili Kachima na wapili kulia  ni SSP Dkt. Richard Mwakina kutoka kituo cha afya chama magereza Ukonga, Dar es Salaam.
Washiriki wa kikao wakifuatilia hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) katika kikao cha waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza nchini kilichoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free  kwa ajili ya ufuatiliaji wa mwenendo  wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18 kilichofanyika leo tarehe 04 Desemba, 2018 jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Gereza Kuu Butimba Mwanza ASP. Dkt.  Alex Lukuba akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi (CGP Kasike) ikiwa ni utambuzi wa kufanya vizuri kwa kituo anachokisimamia katika kusimamia masuala yahusuyo Ukimwi katika kituo chake. 
Kamishna Jenerali wa Magereza  (CGP) Phaustine Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza kote nchini na watendaji wakuu wa Asasi ya isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free ambayo ndiyo wafadhili wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya Magereza na polisi nchini. (Picha zote na Jeshi la Magereza)

Na ASP Deodatus Kazinja, Dodoma.
Wataalam wa  afya wa vituo vya magereza nchini wameaswa kufanya kazi kwa weledi na juhudi kubwa ili kutimiza malengo yanayotarajiwa na jeshi la magereza na taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku moja wa waganga wakuu wa vituo vya afya vya Jeshi la Magereza uliofanyika katika Ukumbi wa Morena Hoteli leo jijini Dodoma.
Aidha, CGP Kasike amemuagiza Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza kufuatilia kwa ukaribu utendaji wa kituo kimoja kimoja na kuhakikisha wataalam waliopo jeshini wanafanya kazi zao kwa uweledi ikiwa ndiyo matarajio ya jeshi.
Wakati huo huo CGP amewatolea wito wataalam hao wa afya magerezani kuhakikisha wanatekeleza muongozo wa serikali unaoagiza kuwaanzishia dawa watu wote wanaogundulika kuwa na maambukizi ya VVU na kuhakikisha wanakuwa na ufuasi mzuri wa dawa.
Waganga wakuu wa vituo vya afya katika Jeshi la magereza wapo katika mkutano huo  unaofadhiliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free  ukiwa na lengo la kufanya tathmini ya mwenendo wa Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18.
Asasi ya JSI AIDS Free chini ya serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani na Wziara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa miaka minne sasa imekuwa ikishirikia na Jeshi la Magereza katika kuboresha Huduma za Afya hasa mapambano ya Ukimwi.

No comments: