Advertisements

Thursday, December 6, 2018

SERIKALI KUIMARISHA UHUSIANO NA NCHI YA FALME ZA KIARABU

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Hafla ya Kusheherekea miaka 47 ya Siku ya Taifa la Nchi ya Falme za Kiarabu, lililofanyika katika Ubalozi wa nchi hiyo, jijini Dar es Salaam. Ambapo aliahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Nchi ya Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu. 
Makamu wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal akichagua tiketi ya mchezo wa bahati nasibu iliyoendeshwa wakati wa Hafla ya Kusheherekea miaka 47 ya Siku ya Taifa la Nchi ya Falme za Kiarabu, lililofanyika katika Ubalozi wa nchi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia) na Viongozi wengine wa Ubalozi wa Nchi ya Falme za Kiarabu wakimkabidhi Ali Suleiman Ali ,zawadi ya tiketi ya ndege kwenda nchini Dubai na kurudi baada ya kuibuka mshindi katika bahati nasibu iliyochezeshwa wakati wa Hafla ya Kusheherekea miaka 47 ya Siku ya Taifa la Nchi ya Falme za Kiarabu, lililofanyika katika Ubalozi wa nchi hiyo, jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal (wapili kushoto), akiongozana na Balozi wa Nchi ya Falme za Kiarabu hapa nchini, Khalifa Abdulrahman Mohamed Al- Marzooqi (watatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kushoto) na wageni waalikwa wakitoka nje ya ukumbi baada ya kumalizika Hafla ya Kusheherekea miaka 47 ya Siku ya Taifa la Nchi ya Falme za Kiarabu, lililofanyika katika Ubalozi wa nchi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Balozi wa Nchi ya Falme za Kiarabu ,Khalifa Abdulrahman Mohamed Al- Marzooqi (kulia), baada ya kumalizika kwa Hafla ya Kusheherekea miaka 47 ya Siku ya Taifa la Nchi ya Falme za Kiarabu, lililofanyika katika Ubalozi wa nchi hiyo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments: