ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 3, 2018

UN yahimiza mapambano dhidi ya UKIMWI

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez alipowasili katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma katika hafla ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018. 
 Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng alipowasili katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma katika hafla ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama.
 Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng (katikati) pamoja na Mratibu wa UKIMWI Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bi. Getrude Sima (wa tatu kulia) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wengine wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakisubiria kuwasili kwa Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutembelea banda hilo wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, RPC Gilles Muroto (kulia) akisalimiana na Mratibu wa UKIMWI Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bi. Getrude Sima (katikati) alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa lililokuwa likionyesha shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng na wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.
 Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na UN nchini wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng  kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na UN nchini alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi jijini Dodoma. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama.
 Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa akihutubia wananchi (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akitoa salamu kutoka wa wahisani wa maendeleo wa UKIMWI wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana wa wizara hiyo wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaosihi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA), Bi. Leticia Mourice akitoa salamu za baraza hilo kwa mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma. 
Baadhi ya washiriki wakiwemo wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dodoma, Maafisa wa jeshi la Polisi, wakazi wa jiji la Dodoma, Wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za serikali, viongozi wa dini pamoja wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa waliohudhuria hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma. 
 Kikundi cha ngoma za asili cha Hiari ya Moyo (Mwinamila) kikitoa burudani ya nyimbo za kuelimisha umma kuhusu masuala ya VVU kupitia sanaa ya ngoma wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma. 
 Mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.  Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko (wa nne kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama (wa tano kushoto),  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kulia) na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Mh. Mussa Sima (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaosihi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA), Bi. Leticia Mourice (kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng (wa tatu kushoto). Mkakati huo unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023.
 Mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez nakala ya Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile. Mkakati huo unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023.
 Mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng nakala ya Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakishuhudia tukio hilo. Mkakati huo unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023.
 Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng wakionyesha nakala ya Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau wa maendeleo wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kitaifa yalifanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa umesema jamii ina wakati mgumu wa kutengeneza mikakati ya kumaliza tatizo la UKIMWI ifikapo mwaka 2030 au la kizazi kijacho kitabeba mzigo mzito wa kuendelea kupambana na janga hili la kidunia. Tamko hilo limetolewa wakati inatambulika kwamba watu milioni 77 duniani wameambukizwa UKIMWI huku wengine milioni 35 wakiwa wamekufa kutokana na magonjwa nyemelezi. Kauli hiyo imetolewa juzi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani, akikariri waraka wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye siku hiyo.

Alisema miaka 30 tangu kuanzishwa kwa siku ya UKIMWI duniani, bado hali ni tete na kwamba juhudi zozote tunazochukua sasa zinaweza kuonesha kama tutazika UKIMWI ifikapo mwaka 2030 au la. Alisema pamoja na dunia kupiga hatua kubwa katika kung’amua na kutibu ugonjwa huo, hatua zilizofikiwa bado hajazifikia nia ya dunia ya kuondokana na tatizo hilo.
Katibu Mkuu huyo alisema kwamba maambukizi mapya hayapungui kwa jinsi dunia inavyotaka huku baadhi ya maeneo yakiwa nyuma zaidi huku raslimali fedha zikizidi kupungua.

Pia hali ya unyanyapaa inazidi kuwa mbaya zaidi na huduma kwa wahitaji zikiwa za kibaguzi na kusababisha kutokuwapo kwa uwazi. Katibu mkuu huyo alitaka dunia kubadilika kuondokana na unyanyapaa na ubaguzi na kuhakikisha kwamba huduma zinatolewa kuudhibiti na kuumaliza ugonjwa huo. Akizungumza katika siku ya UKIMWI mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI na kusema UN ipo sanjari na juhudi za Tanzania.

Alisema amefurahishwa na ukweli kuwa mipango mikakati iliyofanywa na serikali pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa umeleta pamoja wadau wengi katika mapambano hayo na kuwezesha kupata dola milioni 550 kutoka Global Fund zitakazotumika katika mpango kazi wa mwaka 2018 hadi 2020.  Alisema kwa kushirikiana na TACAIDS na uongozi wa udhibiti wa UKIMWI nchini Umoja wa Mataifa na wadau wengine wamewezesha Tanzania kupiga hatua katika kukabiliana na maambukizi mapya.

Aidha alisema kampeni mbalimbali hasa za wanaume zimeanza kufanikiwa na kwamba elimu inayotolewa inafanya wananchi kuwa wazi na kutafuta huduma za kupima na dawa ili kuwa na taifa lenye afya. Mratibu huyo alisema kwamba Umoja wa Mataifa uko tayari kuendeleza ushirikiano wake na Tanzania ili ifikapo mwaka 2030, UKIMWI usiwe tishio. Alisema hilo litawezeka na kwa kuendelea kufanya kazi na serikali na wadau mbalimbali Kwanza,katika harakati za kuzuia maambukizi mapya, Pili: kuondoa kabisa mambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwa mtoto na tatu kupunguza ukatili wa kijinsia na kusaidia upatikanaji wa huduma za afya zinazohusiana na UKIMWI kwa ujumla.

Naye  Dk Leo Zekeng, ambaye ni Mkurugenzi mkazi wa Shirika la UNAIDS alisema amefurahishwa na kuwapo kwa utashi wa kisiasa kukabiliana na maradhi ya UKIMWI kutokana na serikali kutumia mbinu mbalimbali kushawishi  uelewa na uwazi. Alisema shirika lake litaendelea kufanyakazi na Tanzania katika kuwezesha kupatikana kwa ruzuku mbalimbali za kusaidia kukabiliana na maambukizi ya UKIMWI. Alisema kutokana na juhdui za pamoja kati ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania watanzania wanakufa kwa sababu ya maambukizi yamepungua kwa asilimia 70 kutokana na tiba za kufubaza virusi vya UKIMWI.

Alisema kuna watanzania 1,000,000 wanaotumia dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI na kwamba lengo ni kuwa na asilimia 95 ya watu wanatambua hali zao za kiafya. Na kwamba 95% yao wanatumia dawa huku asilimia 95 wanaotumia dawa wakifanikiwa kufubaza virusi hivyo. Pamoja na kufurahishwa na serikali kuruhusu kujipima wenyewe HIV Dk Leo ametaka jamii kuhakikisha inajikita kukabilina na maambukizi ya UKIMWI.
Wakati huo huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba serikali ya Rais John Magufuli itaendelea kutekeleza na kuboresha huduma za upimaji wa Virusi vya UKIMWI, kuzuia kabisa maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, matibabu ya magonjwa nyemelezi pamoja na kupiga vita unyanyapaa wa aina zote kwa WAVIU.

Hata hivyo ametaka kila mmoja katika nafasi yake kuendelea kuwakumbusha wanaoishi na VVU (WAVIU)kuendelea kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU bila kuacha. Pia aliitaka jamii jamii kutowanyanyapaa au kuwabagua WAVIU huku akitoa wito kwa watu wote hususan wanaume kujitokeza kupima ili wajue hali zao.

No comments: