Advertisements

Friday, December 7, 2018

WAZIRI MHAGAMA AAGIZA HALMASHAURI KUSHIRIKISHA WATU WENYE ULEMAVU PROGRAMU YA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa vijana na wakazi wa Mkoga alipofanya ziara ya kikazi Mkoa wa Ruvuma na Iringa kwa lengo la kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi na kutoa mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya Kilimo cha kitalu nyumba.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Bw. Ahmed Njovu akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Mkoani humo.
Afisa Maendeleo ya Vijana Bw. Atilio Mgamwa akitoa taarifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama juu ya hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa programu ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba
Mratibu wa Mradi wa Kitalu Nyumba Bi. Elizabeth Kalilowele akielezea utekelezaji wa mradi wa kitalu nyumba ulipofikia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.
Baadhi ya Watendaji, vijana na wakazi wa Mkoga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo na ujenzi wa kitalu nyumba
Baadhi ya Watendaji, vijana na wakazi wa Mkoga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo na ujenzi wa kitalu nyumba
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mkoga (kulia) akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kitalu Nyumba
Muonekano wa eneo moja wapo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba (Green House).

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

iri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameagiza halmashauri zitakazojengwa vitalu nyumba kushirikisha vijana wenye ulemavu.

Waziri Mhagama ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma na Iringa kukagua maeneo yatayojengwa na kutoa mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba (Green House).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo alisema kuwa katika halmashari zote 83 ambapo teknolojia ya kilimo cha kitalu nyumba itaanzishwa, idadi ya vijana 100 watakaopata mafunzo hayo ijumuishe na wenye ulemavu.

“Halmashauri zitengeneze mfumo madhubuti wa kuwashirikisha vijana wenye ulemavu katika mradi huu, kwani wanaouwezo wa kufanya kazi kama ilivyo vijana wengine na wakiwezeshwa wanaweza”, alisema Mhagama.

Pamoja na hayo, Mhagama amehimiza halmashauri hizo zisimamie vyema mradi huo kwa kuufanya unakuwa endelevu na kuwaunganisha vijana kwenye vyama vya akiba na mikopo ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kujiendeleza kiuchumi kupitia programu hiyo.

Aliongeza kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu imeshakamilisha maandalizi yote ikiwemo wataalamu watakao fundisha vijana kujenga kitalu nyumba, kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji, upandaji wa miche na kuwaelimisha mifumo mizuri ya kutafuta masoko.

Naye, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bw. Lucas Kambelenjo amemuhakakikishia Mhe. Waziri kusimamia ipasavyo mradi huo na kuahidi kutekeleza maagizo aliyoyatoa pamoja na kuwahamasisha vijana zaidi kushiriki katika kujifunza teknolojia hiyo mpya ya kilimo cha Kitalu Nyumba.

Waziri Mhagama alifanya ziara hiyo Mbinga Mji eneo la Mji Mwema, Nyasa na Mkoga, Iringa. Mradi huo unategemea kuanza kwenye Mikoa 12 ikiwemo ya Dodoma, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera, Manyara, Lindi, Shinyanga na Kilimanjaro.

No comments: